AFISA TARAFA KATERERO, POLISI KATA WAPITA VIJIWE VYA BODABODA KUTOA ELIMU USALAMA BARABARANI - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 5 October 2025

AFISA TARAFA KATERERO, POLISI KATA WAPITA VIJIWE VYA BODABODA KUTOA ELIMU USALAMA BARABARANI

Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Bwanku Bwanku (katikati mwenye suti nyeusi) pamoja na Mkuu wa Polisi wa Kata ya Kemondo, Huruma Kulinganila (mwenye sare za Polisi) na maafisa watendaji kata wakiwa kwenye ziara ya kutembelea vijiwe vya bodaboda na kutoa elimu ya usalama barabarani.

................................

Na Mwandishi Wetu, Kagera

AFISA Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Bwanku Bwanku pamoja na Mkuu wa Polisi wa Kata ya Kemondo, Huruma Kulinganila na maafisa watendaji kata wamefanya ziara ya kutembelea vijiwe vya bodaboda na kutoa elimu ya usalama barabarani.

Akizungumza na vyombo vya habari Bwanku Bwanku alisema wamefikia hatua hiyo ili kukabiliana ajali za pikipiki ambapo ndani ya kipindi kisichozidi miezi miwili kata hiyo imeshuhudia ajali tatu za barabarani zilizoua watu watatu.

“Tumeamua kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda ili kukailiana na ajali za barabarani ambazo zinatia maisha ya watu ambao ni tegemeo kwa familia zaona taifa kwa ujumla,” alisema Bwanku.

Timu hiyo iliwahimiza waendesha bodaboda kuacha kuendesha pikipiki zao kwa mwendo wa kasi na kuwataka kuvaa kofia ngumu maarufu kama helmet ili ajali inapotokea ziweze kupunguza madhara kwa binadamu.

Aidha, katika ziara hiyo waliwahimiza waendesha bodaboda hao pamoja na wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu hasa nyakati hizi Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu na kupuuza wale wote wanaohubiri maandamano na machafuko.

Bwanku Bwanku akisisitiza jambo wakati wa utoaji wa elimu.
Wananchi wakisikiliza kwa makini elimu hiyo
Elimu ikitolewa
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad