Kwa muda mrefu nilikuwa mtu wa kawaida tu ambaye alifurahia kurudi nyumbani jioni, kula chakula cha jioni, na kupata usingizi wa amani. Lakini ghafla maisha yangu yalianza kubadilika kwa namna ambayo sikuielewa. Ilianza taratibu.
Usiku mmoja niliota ndoto ya kutisha sana kiasi kwamba niliamka nikitetemeka. Mwanzoni nilipuuzia nikijua kila mtu huota ndoto mbaya wakati mwingine.
Lakini siku zilizofuata hali ilianza kuwa tofauti
.
Karibu kila usiku nilikuwa naota ndoto zilizoniacha na hofu kubwa. Wakati mwingine nilikuwa naamka ghafla katikati ya usiku moyo ukidunda kwa nguvu, nikashindwa hata kurudi kulala. Nilianza kuogopa kufunga macho.



0 Comments