Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuviakimkabidhi ripoti ya utatuzi wa migogoro hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge.
Moja ya Tanki kwenye mradi wa visima vya maji katika mtaa wa Mwankoko likikaguliwa.
Na Dotto Mwaibale Singida
MAWAZIRI nane
wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
hatimaye wameanza rasmi ziara ya kutembelea mikoa 10 ikiwemo Singida kwa ajili
ya kutoa matokeo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 920.
Wakiwa mkoani
Singida leo Oktoba 8, 2021 Lukuvi alisema ziara hiyo ni utekelezaji wa maagizo
ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi
kwenye vijiji na mitaa 12 ambavyo wananchi wake walivamia maeneo ya hifadhi za
misitu, mashamba na mifugo ndani ya Mkoa wa Singida.
" Tuneleta
timu ya kufanya tathmini, kiweka alama na mipaka inayoonekana ili kujua kiwango
cha ardhi kinachotakiwa kutumiwa na wananchi waliopo katika maeneo hayo,"
alisema Lukuvi na kuongeza;
"Suala la
kuwa na wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi je wabaki au wasibaki hilo
limeshamalizwa na Mheshimiwa Rais Samia kwamba wabaki wasiondolewe."
Alifafanua mantiki
ya ziara hiyo alisema katika kujua wananchi hao wanabakije suala la uungwana
linahitajika ambalo ni wao kujiridhisha kwa kufanya tathmini kwa ardhi
waliovamia ili ardhi itakayobaki ilindwe kwa mujibu wa sheria.
Ziara hiyo imekuja
kutokana na baadhi ya hifadhi kuonekana kukosa sifa na Serikali kuamua wananchi
wabaki katika maeneo hayo kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge alisema, ofisi
yake sasa itahakikisha inasimamia pamoja na kuifatualia migogoro yote ya ardhi
ikiwemo ile ya mipaka katika wilaya na vijiji ili kumaliza kabisa migogoro ya
ardhi.
Wakiwa katika Manispaa ya Singida Mawaziri hao wametembelea eneo
la Mwankoko lenye mgogoro ulioanza mwaka 2016 kati ya Mamlaka ya Maji na
Usafi wa Mazingira Mjini hapa (SUWASA) na wananchi wanaolalamikia
kupunjwa fidia waliyolipwa na Serikali ili kupisha utekelezaji wa mradi mkubwa
wa maji wa Mwankoko ambapo baada ya Mawaziri kusikiliza pande zote mbili,
Mwenyekiti wa Kamati wa Mawaziri wa Kisekta ambaye pia ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi amemwagiza Mthamini Mkuu wa
Serikali kufika mkoani hapa siku ya Jumatatu ya wiki ijayo ili kufanya
uchunguzi na kujua ukweli kuhusu malalamiko hayo.
Mawaziri hao wa
kisekta waliokuwa kwenye ziara hiyo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, TAMISEMI, Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mazingira, Utalii, Ulinzi na Maji.
Hata hivyo kwa mujibu wa Lukuvi timu hiyo mawaziri baada ya Singida inatarajia kuendelea na ziara hiyo kwa awamu ya kwanza katika mikoa mingine ya Tabora, Manyara, Mbeya, Morogoro, Geita, Mara, Dar es Salam na Pwani.
0 Comments