MANDONGA KUJA NA NGUMI YA SGR PAMBANO LA NGUMI YA TANGA

Subscribe Us

MANDONGA KUJA NA NGUMI YA SGR PAMBANO LA NGUMI YA TANGA

Na Oscar Assenga, TANGA.

BONDIA wa Ngumi nchini Karim Mandonga ametamba kuonyesha Ngumi ya SGR katika Pambano la Ngumi ya Tanga litakalofanyika Novemba 16 likiwa ni kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.

Mandonga aliyoa tambo hizo wakati wa mkutano na waandishi wa Habari kuelekea pambano hilo ambalo ni moja ya mapambano ambayo yameandaliwa na Kampuni ya Ngumi za Kulipwa ya Mafia Boxing Promotion yatakayofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani Mjini Tanga ambapo Alisema kwamba unapigwa ngumi Tanga unakwenda kuzindukia Dar

Alisema kwamba ngumi SGR ni zawadi ya Rais Dkt Samia Suluhu ambayo anatarajia kuionyesha kwenye pambano hilo ambalo linatarajiwa kushirikisha mabondia wakali na wenye uwezo mkubwa wa kupambana wanapokuwa jukwaani.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo ,Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhary Kubecha amesema pambano hilo ni kwa ajili ya ngumi na kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.

Aliwapongeza kwa kuelekea pambamano hilo ambalo limeandaliwa na Mafia Boxing Promotion kwa kushirikiana na Ofisiy a Mkuu wa wilaya yenye lengo mahususi la kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa 27 Novemba 2024.

Alisema kwamba Mafia wamekuwa ni wadau wakubwa Tanga na Tanzania kwa ujumla katika kukuza vipaji vya mabondia kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali hivyo walipokuwa na wazo lao waliniomba washirikiane waliandae hapa Tanga na waliridhia waliandae pambano hilo ambalo litashirikisha mapambano tofauti tofauti .

Aidha aliwaomba wadau wa ngumi nchini na pembezoni wasipange kukosa hiyo ni ngumi ya Tanga ambayo inahamasisha wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku akiwataka wananchi wajitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.

Alisema kwamba kauli mbiu ngumi yetu ni kura yangu uchaguzi wangu maendeleo yangu tushiriki kwenye uchafguzi wa Serikali za Mitaa.

Hata hivyo alisema kwamba hamasa ya uchaguzi kwa wananchi ni kubwa wasipange kukosa pambano hilo kwani wanataka liwe la kihistoria na wao wamejiandaa vizuri na pambanano hilo litakwenda kuwa la aina yake.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba kwaa upande wake Serikali wamejipanga vilivyo katika suala la usalama kwa pambano hilo na mchezo huo sio wa vita ni urafiki na unajenga umoja na mshikamano .

Alisisitiza pia kwamba mchezo wea ngumi sio uadui bali ni mchezo kama ilivyo michezo mingine wataendelea kuwaunga mkono na Mafia Boxing Promotion wamekuwa wadau wakubwa ya ngumi nchini.

Hata hivyo aliwashukuru Mafia Boxing Promotion kwa kuja na mpango wao wa kugawa majiko ya gesi 500 waliyoyagawa kwa wananchi na wamekuwa wadau wakubwa kurejesha kwa jamii na wanajivunia uwepo wao ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu ya kuhamasisha matumishi ya nishati safi ya kupikia ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba alimpongeza Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha kwa maono yake na kusingekuwa na pambanano kama sio yeye.

Alisema na hivyo ndio sifa pekee ya kiongozi lazima uwepo na maono wanayojivunia kuwa na kiongozi mzuri mwenye maono mazuri jambo ambalo limepelekea na wao kuandaa kitu ambacho kitainua zoezi la upigaji wa kura.

Hata hivyo alisema kwamba wanamshukuru sana na wanaamini wataendelea kushikiana naye kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo na wanatarajia kesho watapokea wageni kutoka Dar na leo watapokea Nje ya nchi lengo la na madhumuni ni kushiriki kwenye pammbano.

Zayumba alisema kweamba wanaendelea kuwakumbusha watanzania kwamba ifikapo Novemba 27 mwaka huu kila mtanzania akikishie anakwenda kutekeleza haki yake ya msingi ya kupigia kura na kutekeleza haki hiyo na wasiipoteze huku akiendelea kusisitiza bado wataendelea kurejeshaji wa jamii jambo ambalo litakuwa endelevu.

Post a Comment

0 Comments