Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba
akiongoza mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili bajeti
iliyopita na ya mwaka huu 2024/2025 uliofanyika Januari 26, 2024 . Kutoka
kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Manyoni, James Mchembe, Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, John Mgalula na Naibu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Jonathan Dule.
..........................................................
Na Dotto Mwaibale, Itigi
HALMASHAURI ya Wilaya ya Itigi katika mwaka
wa fedha wa 2022/2023 imejivunia kupata mafanikio lukuki ambapo katika
bajeti ya 2024/2025 imeomba kuidhinishiwa jumla ya Sh.Bilioni 19.9 kwa ajili ya
kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo.
Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Emmanuel
Dyelu akizungumza katika mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili
bajeti iliyopita na ya mwaka huu uliofanyika Januari 26, 2024 alisema makadirio
ya Mipango na Bajeti kwa Mwaka 2024/25 kuwa fedha hizo zitajumuisha Sh. Bilioni
13.5 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh.Bilioni 6.4 kwa ajili ya shughuli
za maendeleo.
Afisa mipango huyo akitoa mchanganuo wa
bajeti hiyo alisema vyanzo huru vya mapato ya halmashauri hiyo makisio yake ni
Sh.Bilioni 1.6 na kwamba vyanzo lindwa ni Sh.Milioni 426.8 huku jumla ya mapato
ya ndani makisio yake yakiwa ni Sh.Bilioni 2.1.
Alisema Ruzuku ya matumizi mengineyo ya
Serikali Kuu makisio yake ni Sh.Bilioni 1.1 na Ruzuku ya matumizi ya mishahara
Serikali Kuu ni Sh.Bilioni 3.3 na kuwa jumla ya ruzuku hiyo ikiwa ni Sh.Bilioni
15 na wadau wa maendeleo ikiwa ni Sh. Bilioni 2.8.
Aidha, Dyelu alisema kuwa jumla ya ruzuku
hiyo ni Sh.Bilioni 17.8 na jumla Kuu ikiwa ni Sh.Bilioni 19.9.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,
Hussein Simba akizungumzia baadhi ya mafanikio waliyopata katika mwaka wa fedha
wa 2022/ 2023 alisema ni ujenzi wa nyumba ya kisasa ya mkurugenzi mtendaji,
kufanya ziara ya kujifunza biashara ya hewa ya ukaa katika Halmashauri ya
Wilaya ya Tanganyika kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri, ununuzi wa
vishikwambi 20 kwa ajili ya uendeshaji wa vikao kidigitali na usajili wa shule
25 za msingi na tatu za sekondari (Majengo, Kitaraka na Mwamagembe)
Alitaja mafanikio mengine kuwa ni ujenzi wa
sekondari mpya ya Majengo, kukamilisha ujenzi wa maabara tatu katika Shule za
Sekondari ya Mitundu, Sanjaranda na Handu na kukamilisha ujenzi wa Hosteli moja
Sekondari ya Mitundu na mabweni mawili Sekondari ya Mgandu na Ipamuda.
Mafanikio mengine ameyataja ni ukusanyaji wa
mapato mzuri ambapo wamefikia asilimia 82 katika mapato huru lakini mapato
lindwa ambayo yakichanganywa yanafikia asilimia 70.
Alisema katika robo mbili walizozifanyia kazi
wana kwenda vizuri na kuwa hata katika sekta ya elimu wapo vizuri kwani
kimkoa ni wa tatu.
Simba alitumia nafasi hiyo kumshukuru
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, John Mgalula pamoja na timu yake ya
wataalamu kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato hasa katika bajeti ya mwaka
huu ambayo ipo vizuri na usimamizi mzuri wa miradi licha ya kuwepo kwa
changamoto ya kuifikia kutokana na baadhi ya barabara kushindwa kupitika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo, John Mgalula aliahidi kukamilisha shughuli zote za maendeleo
ikiwa ni pamoja na kupeleka madawati Shule ya Msingi Mwamagembe huku akiwaomba
wananchi wa Kata ya Mwamagembe kuandaa eneo lenye ukubwa wa ekari 50 kama
inavyotakiwa na kuanzisha ujenzi wa kituo cha afya kwa kutumia nguvu za
wananchi na kuwa halmashauri hiyo itawaunga mkono.
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wilaya ya Manyoni, Maimuna Likunguni, alipongeza Baraza la Madiwani chini ya
Mwenyekiti Hussein Simba kwa namna linavyo simamia vizuri utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo inayotokana na fedha nyingi zinazotolewa na Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan ambayo inaonekama kwa ubora na thamani halisi ya fedha
zilizopokelewa.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini ni Vijijini Halmashauri ya Itigi, Ndilanka Bukwimba alisema katika mwaka wa fedha 2024/2025 wametenga Sh.Bilioni 3.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara katika halmashauri hiyo.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, John Mgalula akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Emmanuel Dyelu akiwasilisha mpango wa bajeti ya mwaka 2024/ 2025 katika mkutano huo.Madiwani wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wakuu wa idara na wataalamu wakiwa kwenye mkutano huo.Wakuu wa idara na wataalamu wakiwa kwenye mkutano huo.Katibu Tawala Wilaya ya Manyoni, James Mchembe, akichangia jambo kwenye mkutano huo.Diwani wa Kata ya Itigi Mjini, Ally Minja, akichangia jambo kwenye mkutano huo.Diwani wa Kata ya Idodyandole, William Masaka, akizungumza kwenye mkutano huo.Diwani wa Viti Maalumu, Eliza Kidolezi akichangia jambo kwenye mkutano huo.Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Mitundu, Rose Madumba, akizungumza kwenye mkutano huo.Naibu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Jonathan Dule. akizungumza.Diwani wa Kata ya Rungwa, Said Yahaya, akizungumza kuhusu ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Stendi ya Mabasi ya Kata hiyo.Diwani wa Kata ya Mgandu, Martin Kaponda, akizungumza kwenye mkutano huo.Madiwani wakiwa kwenye mkutano huo.Wataalamu na Wakuu wa Idara wakiwa kwenye mkutano huo.Diwani wa Kata ya Ipande, Kedmon Mponda, akizungumzia kuhusu ujenzi wa shule ya Msingi ya Dimwelu.Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini ni Vijijini Halmashauri ya Itigi, Ndilanka Bukwimba, akizungumzia kuhusu utekelezaji wa miundombinu ya barabara katika mwaka huu wa fedha.Katibu wa CCM Wilaya ya Manyoni Maimuna Likunguni, akichangia jambo wakati akitoa salamu za chama kwenye mkutano huo.
---ANGALIA VIDEO---
0 Comments