MWENYEKITI wa hHalmashauri ya Wilaya ya Uyui
mkoani Tabora Said Ntahondi amekanusha tuhuma akidaiwa kuanza kampeni za
kuwania ubunge jimbo la Tabora Kaskazini 2025.
Ilidaiwa
kuwa amekuwa akifanya kampeni za kuwania nafasi hiyo kinyume na taratibu
na kanuni za chama cha mapinduzi zinavyoelekeza kwa wanachama wake kwa kuwa
muda wa kufanya hivyo bado haujafika.
Akizungumza juu ya madai ya
kudaiwa na baadhi ya wana CCM wenzake
kusambaza uvumi kuwa yeye ameanza kujipitisha ili kufanya ushawishi ili aweze
kupata nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Tabora Kaskazini Ntahondi alisema kuwa
huo nu uzushi unaolenga kumchafua kisiasa.
“Mimi nachofanya ni kufanya ziara ya kikazi kwa
mujibu wa nafasi yangu kama mwenyekiti wa halmashauri kusaidia na kukagua
miradi ya maendeleo kama ilani inavyoagiza” alisema.
Mwenyekiti huyo alifafanua kuwa kinachosemwa
dhidi yangu ni uzushi na majungu dhidi yake na baadhi ya viongozi ambao hakuwa
tayari kuwataja.
Alisema anafahamu taratibu za CCM katika chaguzi
zote hivyo kufanya kitu kinachoenezwa ni kinaitwa utoto kwenye uongozi au
kuwania nafasi yoyote ile ndani ya CCM kwani yeye anajitambua.
Aliongeza kuwa kuna baadhi ya viongozi wanaomchafua na kuongeza
kwamba muda ukifika kwa mujibu wa
taratibu za chama hicho kama atatota taarifa lasmi kama atawania ubunge au
udiwani katika kata yake ya Isila ambako kwa sasa ndiyo yeye ni ndiye diwani wa
kata hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Tabora
Kaskazini Almas Maige alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo dhidi ya mwenyekiti
wake wa halmashauri alisema hawezi kuzungumzia lolote juu tuhuma hizo na
kuongeza kuwa anatambua wapo baadhi ya watu walioanza kujipitishapitisha
kulitaka jimbo hilo.
Maige alifafanua kuwa Katibu wa Itikadi siasa na Uenezi Taifa Paul Makonda alishakemea na kusema wanachama ambao walishaanza
kujipitisha waache mara moja na watakaobainika watachukuliwa hatua za
kinidhamu.
“Mimi bado ni Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini,
hivyo wanajipitisha wasubiri muda ukifika ndipo wataruhusiwa kuomba nafasi za
ubunge ama udiwani kwa mujibu wa taratibu,kanuni na miongozo ya chama chetu “
alisema Maige.
Aidha alisema kuwa chini ya nafasi yake amefanya
mengi mazuri akiwa mbunge wa jimbo la Tabora Kaskazini ikiwemo ujenzi wa
barabara,ujenzi wa shule zikiwemo za kidato cha tano na sita,hospitali ya
wilaya na kwamba anaishukuru serikali ya awamu sita chi ya Dkt Samia Suluhu
Hassan kwa kupokea zaidi y ash bilioni 53 kwa ajili ya miradi ya maendeleo
katika jimbo lake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Uyui Rubasha Makoba alipoulizwa madai hayo alisema hadi sasa
hajapokea wala kupata malalamiko yoyote toka kwa diwani wala mbunge ya kuchezwa
rafu kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Aliongeza sisi kama viongozi wa chama tikipata malalamiko ya kimaandishi na kukawa ushahidi huwa tunaachukua hatua za kinidhamu kupitia vikao vyetu vya chama.
0 Comments