Mzee Salumu Mrisho (kulia) wa Kata ya Kintinku akiwa amekumbatiana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kintinku, Mateso Bwire kuonesha ishara ya kumaliza sintofahamu iliyoibuliwa na mzee huyo akidai mwalimu huyo anawazuia watoto wake kwenda kuswali.
...............................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida chini ya Sheikh
wa mkoa huo, Issa Nasoro limefanikiwa kumaliza sintofahamu ambayo ilileta
taharuki baada ya mzazi mmoja wa Kata ya Kintinku Salumu Mrisho kudai kwamba
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kintinku, Mateso Bwire amewazuia watoto wake
wannne ambao ni wanafunzi wa shule hiyo kwenda kuswali siku ya Ijumaa hivyo
kukosa fursa na haki ya kuabudu.
Mrisho alitoa madai hayo baada ya kujirekodi na kuyarusha katika mtandao
jambo ambalo lilileta taharuki miongoni mwa jamii lakini Februari 19, 2024
wajumbe wa BAKWATA Mkoa wa Singida wakiongozwa na Sheikh Issa Nasoro walifika
katika shule hiyo na kuzungumza na walimu na kisha kwenda nyumbani kwa Mzee
Mrisho na kufanya naye mazungumzo ambayo yalileta tija na kumaliza changamoto
iliyojitokeza ambapo wote kwa pamoja wakiwepo walimu wa shule hiyo walishikana
mikono na kufanya dua kuashirikia kuanza maisha mapya yaliyojaa upendo, amani na
mshikamano baina ya pande zote.
Wakati huohuo baada ya kuitatua changano hiyo Sheikh Nassoro aliwaongoza
baadhi ya waislamu wa Manyoni kumfanyia dua ya Mama wa Mwanazuoni Sharif Sayyed Jaafar-Al-beidh, Hababa Ummul-Khayr aliyefariki
Februari 16, 2024 huko Lam Mombasa nchini Kenya.
Akizungumza wakati wa dua hiyo iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa mjini Manyoni
Sheikh Nawawl Salim Itara Mudir wa Chuo cha Jaamiul- Farouq kilichoasisiwa na
Sharif Sayyed Jaafar-Al-beidh alisema kifo cha mama huyo kimewasikitisha
waislam wengi waliokuwa wamemfahamau na ndio maana wameamua kumfanyia heshima
ya kidini kwa kumfanyia dua hiyo kutokana na kazi kubwa anayoifanya mtoto wake
Sharif Sayyed Jaafar-Al-beidh.
Sheikh Itara alisema Sharifu Jaafar ni Mwanazuoni Mkubwa ambaye
anafanyakazi ya kulingania upande wa Afrika Mashariki na Dunia kwa ujumla na
mtu muhimu sana katika kueneza dini ya kiislam.
"Sharifu Jaafar tumekuwa tukishirikiana naye kwa muda mrefu licha ya kuwa yupo nchini Kenya amekuwa akifika hapa Manyoni kila wakati na kujumuika naye mambo mbalimbali ya kiimani," alisema Sheikh Itara.
0 Comments