Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog
SAKATA la baadhi ya viongozi wa Kiislam wa Kata ya Mtinko iliyopo Wilaya
ya Singida kudaiwa kutaka kusajili
taasisi ndani ya Msikiti wa Kata hiyo
ambao upo chini ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) pasipo kujua
limechukuwa sura mpya baada ya kurejeshwa kwenye nafasi zao kufuatia Kamati ya
Baraza la Masheikh Mkoa wa Singida
iliyoundwa kuchunguza jambo hilo kubainika kuwa walikuwa wapo sahihi.
Mwanasheria Mkuu wa Bakwata , Hassan Fatihu
akizungumza na waislamu wa kata hiyo Machi 1, 2024 wakati akitoa taarifa
ya kamati hiyo alisema walibaini wahusika hawakuwa na nia ovu ya kutaka kufanya
mapinduzi ya umiliki wa msikiti huo bali walisukumwa kutaka kuendelea kufanya
maendeleo .
"Baada ya kuwasimamisha viongozi hao tuliunda kamati ya kuchunguza
madai hayo ambapo tulibaini hawakuwa na nia mbaya bali walisukumwa na kufanya
maendeleo ya msikiti huo," alisema Fatihu.
Fatihu alisema kutokana na kutokuwa na weledi wa kutosha kwa baadhi ya
viongozi hasa makatibu kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya ndio waliosababisha
jambo hilo kufikia hatua hiyo na kuleta taharuki miongoni mwao kwani wangeweza
kubaini mapema kuwa msikiti huo tayari ulikuwa upo ndani ya Mamlaka ya Bakwata.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza kwenye kikao hicho cha
kupokea taarifa hiyo aliwataka viongozi wa kiislam kuanzia ngazi ya kata hadi
mkoa kufanyakazi zao kwa kuzingatia katiba ya Bakwata ambayo inaelekeza kitu na
si vinginevyo.
Aidha, Sheikh Nasoro alitumia nafasi hiyo kuwaongoza waislam wa Kata ya Mtinko kwa niaba ya waislam wa Mkoa wa Singida kumuombea dua Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alifariki Februari 29, 2024 majira ya saa 11 jioni katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na mazishi yake kufanyika leo Machi 2, 2024 Unguja Zanzibar.Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akisisitiza viongozi wa Kiislam kufanyakazi zao kwa kufuata Katiba ya Bakwata wakati akizungumza na Waumini wa Kiislam wa Kata ya Mtinko Wilaya ya Singida.Mwanasheria Mkuu wa Bakwata , Hassan Fatihu akizungumza na waislamu wa kata hiyo Machi 1, 2024 wakati akitoa taarifa ya kamati hiyo.Sheikh wa Wilaya ya Singida, Ibrahim Ntandu akizungumza wakati wa kikao hicho.Sheikh Issa Bakar akizungumza kwa niaba ya Umoja wa wana Singida waishio Dar es Salaam ambao ni wadau wakubwa wa maendeleo wa dini ya kiislam katika Kata ya Mtinko na Mkoa wa Singida kwa ujumla. Wadau hao ndio wanaoendelea kuchangia ujenzi wa msikiti huo.Katibu wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Singida, Said Mang'ola akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.Mzee wa Msikiti wa Kata ya Mtinko, Juma Mene, akizungumza kwa niaba ya wazee wa msikiti huo.Mmoja wa Kiongozi wa Taasisi ya Kiislam mkoani hapa Haji Mtulia, akichangia jambo kwenye kikao hicho.Wazee wa Kiislam wa Kata ya Mtinko wakiwa kwenye kikao hicho.Kikao kikiendelea.Kikao kikiendelea.Waumini wa Kiislam wakiwa kwenye kikao hicho.Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza na Waislam wa Kata ya Mtinko.Wanawake wa dini ya Kiislam wa Kata ya Mtinko wakiwa kwenye kikao hicho.Sheikh Issa Nasoro akiwaongoza Waislam wa Kata ya Mtinko kwa niaba ya waislam wa Mkoa wa Singida kumuombea dua Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alifariki Februari 29, 2024 majira ya saa 11 jioni katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu na mazishi yake kufanyika leo Machi 2, 2024 Unguja Zanzibar.
Viongozi waliokuwa kwenye kikao hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa Msikiti wa kata hiyo pamoja na baadhi ya waumini wa Kiislam wa Mtinko.
0 Comments