RAIS SAMIA ATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA SHAMRASHAMRA ZA MIAKA 60 YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Salma Kikwete Nishani ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24
Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu
wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema
yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli
kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24
Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu
wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema
yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja
la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya
Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja
la Pili Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed
Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma
tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja
la Pili Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya
Awamu ya Tatu Mhe. Frederick Tluway Sumaye kwenye hafla iliyofanyika katika
Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
No comments