Wananchi waliotembelea banda la UTT AMIS wakijaza fomu za kujiunga na mfuko huo katika Maonesho ya saba (7) ya kitaifa ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendendelea Viwanja vya Bombadia Manispaa ya Singida Septemba 11, 2024. Kulia anayeshuhudia ujazaji fomu hizo ni Afisa Masoko wa UTT AMIS, Doris Mlenge.
.......................................
Imeandaliwa na Dotto Mwaibale, Solomoni Philemon ( 0754-362990 )
KUANGALIA VIDEO YA TUKIO HILI BOFYA HAPA CHINI
WAFANYAKAZI na wafanyabiashara wametakiwa kujenga mazingira
ya kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadae.
Ombi hilo
limetolewa na Afisa Masoko wa UTT AMIS, Doris Mlenge wakati akitoa taarifa fupi
ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo ya Serikali ambayo ipo chini ya Wizara
ya Fedha kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleimani Mwenda wakati alipokuwa
akitembelea mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya saba (7) ya kitaifa ya mifuko ya
programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendendelea Viwanja vya Bombadia
Manispaa ya Singida.
Mlenge alisema dhumuni kuu la taasisi hiyo ni kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwezeshaji wa pamoja nchini lengo likiwa kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba na kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji.
Aliitaja mifuko hiyo iliyoanzishwa na UTT AMIS kuwa ni mfuko wa umoja, wekeza maisha, ukwasi, mfuko wa watoto, mfuko wa kujikimu ambao alisema lengo la mfuko huo ni kutoa gawio na kukuza mtaji kwa wawekezaji wake kwa muda wa kati na muda mrefu na kuwa unawekeza katika hisa na masoko ya fedha.
Mlenge alisema mifuko hiyo ipo tofautitofauti kutokana na mwanachama anachokitaka kuna uwekezaji kwa wafanyabiasha wadodo wajasiriamali ambao wanashauriwa kuchukua mfuko wa ukwasi .
Alisema faida ya mfuko huo mfabiashara anaweza kuweka na kutoa fedha zake wakati wote na kuwa kupitia biashara wanazozifanya na faida wanazozipata wanawashauri wawekeze ili waweze kutengeneza faida nyingi.
Aidha, Lulenge alisema kupitia uwekezaji huo wanatengeneza faida kwa mwaka sio chini ya aslimia 12.
Alisema kuwekeza mapema ndivyo unavyotoa muda mrefu wa fedha kuwekezwa na kukupa faida zaidina kuwa kila mwaka kiasi kitakachoongezeka (faida) kitazalisha faida nyingine katika miaka itakayofuata faida inazidi kuongezeka na huku mtaji nao ukiongezeka kadri miaka inavyoongezeka.
Mlenge alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kutembelea kwenye banda lao kwa ajili ya kupata elimu mbalimbali za uwekezaji na kujiunga na mfuko huo ambao ni muhimu kwa maisha ya baadae.
0 Comments