Happy Lazaro, Arusha
Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kuharakisha zoezi la upimaji wa maeneo ya ardhi umebainishwa kama suluhisho la kudumu la utatuzi wa migogoro ya ardhi inayoibuka mara kwa mara baina ya wananchi na serikali katika Halmashauri ya Arusha iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Hata hivyo Mkoa wa Arusha unatajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa yenye changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi katika jamii.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Dkt.Ojung’u Salekwa amekieleza kikao cha kawaida cha robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha wa 2024/2025 cha Baraza la madiwani katika halmashauri hiyo kwamba migogoro hiyo inatokana na uhaba mkubwa wa ardhi.
Dkt.Salekwa amesema kuwa,kuwepo kwa matumizi Bora ya ardhi utasaidia sana kuondoa migogoro mbalimbali baina ya wananchi na serikali katika maeneo mbalimbali kwani kila mmoja ataweza kuitambua mipaka take bila kuwepo kwa mwingiliano wowote.
“Naombeni sana madiwani msimamie kikamilifu matumizi bora ya ardhi katika maeneo yenu ili kuondoa changamoto.mbalimbali.kwa.wananchi huku mkiendelea kutoa elimu.zaidi kwa.wananchi wenu kuhusu matumizi bora ya ardhi.kwani wengi wao hawana elimu ya kutosha kuhusu elimu hiyo na nyie ndio mnapaswa kuwapa elimu hiyo.”amesema Dkt.Salekwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Stedvant Kileo ametaja mpango mkakati wa kuongeza nguvu ya ukunyaji wa mapato hususani katika masoko na minada kwa ajili ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kileo amesema kuwa,halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa mapato yanazidi kuongeza kwa kiwango cha juu huku.wakiongeza nguvu zaidi katika ukusanyaji katika vyanzo mbalimbali vya mapato katika halmashauri hiyo.
Kwa upande wao Madiwani wameshauri mwelekeo bora wa kufanikisha mipango mbalimbali kwa ubora unaotarajiwa wa serikali.
Diwani wa kata ya Oltrument ,Joseph Tinayo Mendasa amesema kuwa ,ni wakati sasa wa kila mmoja wetu kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi mbalimbali katika halmashauri hiyo ili ukusanyaji uzidi kupaa zaidi.
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imepaa katika ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilioni 4.8 mpaka bilioni 6.9 kwa mwaka.
0 Comments