Mbunge wa Ruangwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
.......................................................
Na Mwandishi Wetum Ruangwa
Umoja wa Wachimbaji kwenye mgodi wa Namungo uliopo kwenye wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi wamejitokeza na kutangaza kumuunga mkono Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia suluhu Hassan kwa kumlipia fomu ya Urais na fomu ya Ubunge kwa Mbunge wa Ruangwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Wachimbaji hao wamesema hiyo ni sehemu ya shukrani kwa Rais na Mbunge wao, ambapo jumla ya zaidi ya Milioni sita zimetolewa. Wakitoa shukrani kwa namna ambavyo serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani Ruangwa.
Kati ya Milioni sira zilizotolewa, Wachimbaji wamesema Milioni nne kwa ajili ya fomu ya Urais kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Milioni mbili kwa ajili ya fomu ya Ubunge kwa Mbunge wao wa Ruangwa Mhe. Kassim Majaliwa.





0 Comments