Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wanachama wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika (AU-PSC) kujadili hali ya usalama nchini Libya.
Mkutano huo umeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Uganda na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, leo tarehe 24 Julai, 2025 kwa njia ya mtandao ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni wa nchi mwanachama wa Baraza hilo ambalo linaundwa na nchi 15 za Umoja wa Afrika.
Katika Mkutano huo, Bashungwa kwa niaba ya Rais Samia amepongeza Juhudi za Mheshimiwa Denis Sassou Nguesso, Rais wa Jamhuri ya Congo na Mwenyekiti wa AU High Level Committee on Libya, hususani kwa kusimamia The National Reconcilliation Charter ambayo inatoa muongozo wa suluhu ya mgogoro nchini Libya ikiwemo kufanyika kwa uchaguzi, kuimarisha taasisi nchini Libya hususan Jeshi.
Thursday, July 24, 2025
Home
Habari
BASHUNGWA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUJADILI HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA NCHINI LIBYA
BASHUNGWA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUJADILI HALI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA NCHINI LIBYA
Tags
# Habari
Kuhusu - Singidaniblog
Habari
Tags:
Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ni chombo cha habari kinachotoa habari na matukio mbalimbali nchini Tanzania na kokote duniani ,kwa kujali weledi na taaluma ya habari.
KWA MATANGAZO NA HUDUMA YA HABARI, WASILIANA NASI,
0754 362 990.
0688 914 344
Email: singidani77@gmail.com,










No comments:
Post a Comment