DKT BINILITH MAHENGE ANAVYOPAMBANA KUIHESHIMISHA SINGIDA KATIKA HADHI INAYOSTAHILI

Subscribe Us

DKT BINILITH MAHENGE ANAVYOPAMBANA KUIHESHIMISHA SINGIDA KATIKA HADHI INAYOSTAHILI

Mkuu wa Mkoa akizungumza wakati wa ziara yake ndani ya Manispaa ya Singida alipokuwa akikagua miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Singida wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Dk. Binilith Mahenge wakati alipofanya ziara kwenye manispaa hiyo juzi. 


Na Godwin Myovela, Singida


KWA mara ya kwanza Dk. Binilith Mahenge alipotua ndani ya Mkoa wa Singida akitokea Dodoma muda mfupi baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dk. RehemaNchimbi…kitu pekee alichobainini kwamba Singida ambayo ni mkoa wa kimkakati uliopo katikati ya Tanzania mbali ya kujaliwa mandharisafi, vivutio vya asili, ardhi yenye rutuba na utajiri wa kipekee-bado una kitu kimoja unachostahili ambacho ni kuheshimishwa kwa kuitwa Jiji.

Kazi yake kwanza ya Dk. Mahenge ilikuwa ni kufanya ziara ya kukutana na makundi mbalimbali ndani ya mkoa wa Singida, ambapo kwanamna ya kipekee alikutana na wazee wote wa Mkoa wa Singida, viongozi wa dini kupitia umoja wao wa dini mbalimbali, watumishi wa Manispaa na Halmashauri zote, pia alihudhuria baadhi ya vikao vya mabaraza ya madiwani, baadaye alitembelea ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari mkoani hapana kuzungumza na wanahabari wote-lengo likiwa nikujitambulisha na kupata fursa ya kuifahamu vizuri Singida.

Lakini kwa aina ya uongozi wake, binafsi namtazama Mahenge katika jicho la utume na utumishi wa dhati kabisa ndani ya mfumo wa serikali ya Mama Samia ambaye dhamira yake ni kumsaidia Rais kufika kwa haraka pale ambapo huduma za kijamii na ustawi wamaendeleo kwa mustakabali mzuri wa watanzania vinastahili kufikiwa kwa kasi kulingana na mipango ya nchi iliyopo. 

Ninamuona katika usikivu na mwenye kiu kubwa yakupata matokeo kwa haraka yatakayotokana na mipango ya umoja na pamoja-yaani ushirikishwaji.

Katika safari yake ya kuifanya Singida kuwa jiji alianza na hamasa kubwa kwenye kilimo cha alizeti katika muktadha wa ongezeko la tija na uzalishaji, na katika hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliongeza nguvu ya kipekee kwa kutembelea mkoani hapa na kutangaza kampeni ya kuhamasisha kilimo cha alizeti kwa azma chanya ya kufidiaupungufu uliopo wa mafuta ya kula ambao huigharimu serikali takribani shilingi bilioni 474 kila mwaka kwa Mafuta hayo kuagizwa kutoka nje.

Waziri Mkuu aliagiza mikoa ya Singida, Dodoma, Simiyu na mikoa mingine ikiwemo Manyara inayostawisha zao hilo kutoa msukumo wa kipkeekwa kuweka mikakati ya kuhakikisha zaidi ya Tani za Mafuta hayo 375,000 zinazalishwa kwa kuzingatia tija na viwango, jambo ambalo mpaka sasa Dk. Mahenge amekuwa akipambana kuhakikisha agizo la boss wake Waziri Mkuu linafanikishwa kikamilifu.

Ili kutosheleza mahitaji halisi ya mafuta ya kula nchini yanayohitajikani Tani 650,000 kwa mwaka, ambapo kama nchi mpaka sasa kwa takwimu zilizopo kiwango kinachozalishwa ni tani 290,000 pekee ambacho bado hakitoshelezi mahitaji.

Dk. Mahenge anaamini, kama Singida itafanikiwa kuzalisha na kusambaza mafuta hayo angalau kwa nusu ya idadi ya mikoa iliyopo nchini basi ni dalili njema ya mkoa wake kufikia kwa kasi azma ya kuwa na maendeleo makubwa kwa hadhi ya jiji…jambo ambalo anaona ni jepesi na linawezekana-endapo kila mwanasingida kwa idadi na makundi ndani ya jamii atashiriki kikamilifu na kutimiza wajibu wake.

Jambo lingine ambalo ni kigezo muhimu cha kuifikishaSingida kuwa Jiji, kwa mujibu wa Dk. Mahenge, mbali ya maboresho ya miundombinu, huduma za maji safi na salama ya uhakika, umeme, huduma za afya…kubwa niukusanyaji wamapato. Na kupitia ziara zake mbalimbali amekuwa akikumbusha na kuhamasisha watendaji juu ya umuhimu wakukusanya mapato kwa kuainisha vyanzo vilivyopo na kuvisimamia ipasavyo na-kwauaminifu kuhakikisha kila chanzo kinakusanya mapato kwa asilimia 100.

Fuatilia hapa chini maswali yake na majibu aliyokutananayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi yakukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kufanya tathmini ya hali ya uwajibikaji kwa watumishi ndani ya Manispaa ya Singida jana-hasa kwenye maeneo ya takwimu za ukusanyaji mapato:

Mkuu wa Mkoa: Mwekahazina, Mchumi au hata Mkurugenzi nataka unisomee taarifa ya mapato ya Manispaa hii ya Singida ya kila mwezi kuanzia mwezi Julai mwaka huu, mniambie mwezi wa 7 mlikusanya shilingi ngapi, mweziwa 8 hizi..wa 9 natakat akwimutu!

Mkurugenzi, Mchumi na Mweka hazina wa Manispaa: hakuna majibu...ukimya umetawala.

Mkuuwa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri: anaingilia kati kusaidia baada ya wahusika walioulizwa kukosa takwimu hizo kwenye kikao hicho cha Mkuu waMkoa. Anasema kwa mwezi wa Julai Manispaa ilikusanya milioni 226,93522.25, mwezi Agosti ilikusanya milioni 350,868734.39, na mwezi Septemba mapato yalikuwa milioni 395,70304.37.

Mkuu waMkoa: Naomba mpigieni makofi mkuu wetu wa Wilaya. 

Jamani hivi Mweka hazina, Mkurugenzi na Mchumi mnajisikiaje baada ya DC kuwasaidia kutoa takwimu hizi? Ni aibu kubwa kwenu kuja kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa bila ya takwimu, na taarifa hizi za mapato ya manispaa kwa kila mwezi wala hata sio za kwenda kutafuta zinapaswa kuwa vichwani mwenu, 

Mweka hazina upo? inawezekana hiyo nafasi haikutoshi ni aibu, sionafasi yako hiyo…naomba jambo hili lisijirudie tena!

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alimtaka Mweka hazina kumweleza kwa fedha iliyopatikana mwezi Julai ni kiasi gani cha asilimia 10 ambazo ni kwa mujibu wa sheria zimetengwa kwa ajili ya makundi ya wanawake, vijana na wenyeulemavu…namweka hazina alimjibu kwa mwezi Julai walitenga milioni 22.

Mkuu waMkoa: Naambiwa mwezi Agostiasilimia 10 imeombwa lakini mpaka sasa tupo mwezi Oktoba bado haijakamilika,haya twende kwenye asilimia 30 mpaka sasa mmetenga ngapi?

Mwekahazina:tumetengaMheshimiwa.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu: Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wataalamu wetu hawafuati sheria za kibajeti kuanzia mwezi 8, 9 na 10 hakuna fedha yoyote iliyotengwa kwa ajili ya asilimia 10.

Mkuu wa Mkoa: NakuagizaMkurugenzi kufikia mwezi huu mwishoni nataka fedha zote za asilimia 10 kwaJulai, Agosti, Septemba na Oktoba ziwe zimetengwa na hiyo taarifa niipate, hiyo ni kwa mujibu wa sheria hata kama mmekusanya kidogo lazima mzitenge…

Aidha Dk. Mahenge akiwa kwenye machinjio kuu ya Manispaa ya Singida iliyopo eneo la Bomani….baada ya kusikilizakero za machinjio hiyo na kuhoji mapato yatokanayo na chanzo hicho anaagiza machinjio hiyo ihamishiweeneo la Ng’aida Kata yaKisaki ili kupisha makazi ya watu. 

Machinjio hiyo kwa sasa imekosa ubora kutokana na kukithiri kwa kasoro mbalimbali uchakavu wa miundombinu ya machinjio na utiririshaji wa maji taka na mbolea kwenye makazi ya watu  hasakipindi cha mvua.

Post a Comment

0 Comments