Na Calvin Gwabara, Kilosa
MKUU wa Wilaya
ya Kilosa Mkoani Morogoro Alhaji Majid Hemed Mwanga amesema wilaya yake
haitamvumilia wala kumfumbia macho kiongozi au Mwananchi yeyote atakayecheza na
rasilimali za Misitu kwa kufanya kinyume na utaratibu uliowekwa kwenye vijiji
vilivyo chini ya mpango wa usimamizi shirikishi wa Misitu ya Vijiji na vile
ambavyo bado havijaingia kwenye mpango huo.
Wito huo
ameutoa wakati wa ziara aliyoifanya na kamati ya Ulinzi Usalama,Madiwani na
viongozi wa Mashirika ya TFCG na MJUMITA katika Kijiji cha Kitunduweta wilayani
humo ili kujionea namna mashirika hayo
yanavyotekeleza mapango wa isimamizi shirikishi wa misitu kwenye vijiji 20 vya
Wilaya hiyo na kusikia shuhuda na mafanikio na kazi kubwa zilizofanywa na
mashirika hayo katika kufikia mafanikio hayo.
”Kwakweli
kazi kubwa sana imefanywa na wadau wetu Shirika la kuhifadhi Misitu ya asili
Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) na
sasa kazi iliyobaki ni sisi kuhakikisha elimu tuliyoipata inaednelea kuleta
matokeo chanya katika kutunza misitu yetu, na niseme tu kwamba fedha nyingi
mnapata kwenye vijiji lakini naomba mtambue kuwa fedha hizo ni fedha za Umma
zitumike kwa kufuata taratibu zote za matumizi ya fedha za Umma na Ssio
vinginevyo maana ninaz taarifa kuwa baadhi ya viongozi wanatumia fedha hizo
vibaya na kuna vijiji kamati zake kama Kijiji cha Ihombwe imeivunja”
Alisisitiza Alhaj Mwanga.
Mkuu huyo wa
Wilaya aliwataka Wananchi kwenye vijiji hivyo kutowafumbia macho viongozi
wanaovuruga utaratibu mzuri ulioanzishwa bali watoe taarifa kwenye ofisi yake
na mamlaka zingine ili washughulikiwe na kuwasisitiza kuendelea kuhifadhi
misitu hiyo ya vijiji na kuitumia kwa uendelevu na kwa maslahi mapata ya vijiji
na Taifa.
“Nyinyi sasa
ni Walimu maana tumeona wenzenu kutoka kwenye Wilaya ya Ruangwa anakotoka Waziri Mkuu wetu walikuja kujifunza kutoka kwenye Kijiji chenu sasa tuache
kulalamika na kunedelea kulilia mafunzo Zaidi maana tunataka sasa hawa wadau
wahamie kwenye vijiji vingine kwenye wilaya yet una mikoa mingine ili elimu hii
ifike nchi nzima, tunachotaka sasa ni kuona nyinyi mnasonga mbele kama walimu”
Aliongeza Mkuu huyo wa wilaya ya Kilosa.
Alhaj Mwanga amewataka kuacha kusikiliza
maneno ya baadhi ya watu wanaokuja kuharibu misitu na kuharibu taratibu
zilizowekwa wakisingizia kuwa ni maagizo kutoka kwa wakubwa na kuwataka waache
kuwasiliza maana hauna maagizo yoyote yanayotoka juu kwenye kuharibu misitu na
akitokea mtu huyo watoe taarifa haraka ili watu hao wakamatwe na kuchukuliwa
hatua.
Mkuu huyo wa
Wilaya ya Kilosa amewasisitiza viongozi wa Kijiji na kamati za maliasili kila
mmoja kutambua majukumu yake na kuacha kuingilia kwenye majukumu ili kuondaa
migogoro isiyo ya lazima ambayo inatokana na hela wanazozipata kutokana na
mapatoa yanayokusanywa kwenye tozo na fedha za misitu.
Akieleza malengo ya Mradi huo Meneja wa Mradi wa Mkaa
endelevu Charles Lyimo amesema lengo kuu ni kuhifadhi Misitu ya vijiji kikamilifu
kutokana na tafiti kuonesha kuwa kwa mwaka Tanzania tunapoteza hekta 460,000 za
misitu kutokana na shughuli mbalimbali za uchomaji Mkaa, Kuni,Kilimo na Mbao na
kiasi kikubwa cha upotevu huo kinafanyika kwenye ardhi za vijiji katika maeneo
ambayo hayajahifadhiwa.
Ameongeza
kuwa katika kufanikisha hilo Mradi unawezesha vijiji pamoja na Wilaya kuweza
kuziwekea mpango bora wa kusimamia rasilimali hizo za mistu vizuri ili
kunufaika nazo kama vijiji lakini pia Serikali kwa ujumla.
Meneja huyo
wa Mradi amesema lengo la pili ni kuchangia kwenye maendeleo ya Wananchi maana
hiyo ndiyo sera ya Serikali kwamba wananchi wanaoishi pembeni mwa rasilimali za
mistu waweze kunufaika nazo kwa njia endelevu nah ii ni katika kuwaonesha
Wananchi kuona rasilimali hiyo ya misitu ni yao na wana jukumu la kuilinda na
kuihifadh kwakuwa wanapata motisha.
”Kupitia program
hii ya uhifadhi shrikishi wa misitu tunaona kwamba kuna haja ya kuzidi
kuiendeleza na jukumu kubwa tulilonalo hasa katika awamu hii ya tatu ya mradi
huu tayari tumeshaanza kuondoka kwenye vijiji vya awali na wilaya ya Kilosa
sasa tunahamia kwenye wilaya zingine nje ya mkoa wa Morogoro na tumewaachia
halmashauri ya Wilaya ili waweze kuwasimamia na kuratibu hivi
vijiji”Alibainisha meneja wa Mradi.
Katibu wa kamati ya maaliasili ya Kijiji cha Kitunduweta, Leoti
Msoloka amesema kupitia Usimaizi shirikishi wa Misitu ya Kijiji chao wamepata
mafanikio makubwa ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Kijiji, Ukatabati wa vyumba vya
madarasa,Ujenzi wa matundu ya vyoo pamoja na kuwakatia bima ya afya
iliyoboreshwa Wanakijiji wote kijijini hapo ambapo sasa wamenza na ujenzi wa
Zahanati ya Kijiji ili wapate huduma kijijini kwao.
“Faida kubwa
ni kwamba hapo awali tulikuwa hatujui umuhimu wa kuhifadhi Msitu wa Kijiji
lakini baada ya elimu na faida tulizozipata na sasa asilimia tisini ya mapato
yatokanayo na misitu zinatumika kijijini tofauti nah apo awali ambapo asilimia
hizo zilikuwa zinaenda wilayani na sasa tunaweza kuzitumia fedha hizo kulinda
msitu na kunufaisha Kijiji chetu” Alifafanua bwana Msoloka.
Mradi huu wa
uhifadhi shirikishi wa misitu ya vijiji unatekelezwa na shirika la kuhifadhi
Misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii usimamizi wa misitu
Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la USWISI (SDC).
0 Comments