MAJONZI, VILIO, SIMANZI VYATAWALA MISA YA KUMUAGA MWANAHABARI DORIS NTALIAGA MEGHJI MKOANI SINGIDA

Subscribe Us

MAJONZI, VILIO, SIMANZI VYATAWALA MISA YA KUMUAGA MWANAHABARI DORIS NTALIAGA MEGHJI MKOANI SINGIDA

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mwanahabari Doris Ntaliaga wakati wakitoka katika Misa Takatifu ya kumuaga iliyofanyika Kanisa Katoliki Jimbo la Singida jana.

Marehemu Doris Ntaliaga Meghji enzi za uhai wake.

Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda aliyeongoza Misa hiyo akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu Doris Meghji wakati wa mazishi yake.
Mama wa marehemu Doris Meghji, Margareth Malecela akiwa na huzuni kwenye misa hiyo.
Baba wa marehemu Doris, Mzee Meghji akiwa na huzuni kwenye misa hiyo.
Ni vilio na huzuni kwenye misa hiyo.
Misa ikiendelea.
Misa ikiendelea.
Ni huzuni kwenye misa hiyo. Hawa jamaa hawaamini kama mpendwa wao Doris amefariki na hawata muona tena.
Utoaji sadaka ukifanyika.
Misa ikiendelea.
Zoezi la kuaga na kutoa heshima mbele ya mwili wa marehemu likifanyika.
Mama wa marehemu Doris Meghji, Margareth Malecela akimuaga mwanaye.
Ni vilio na huzuni wakati wakitoka kwenye misa hiyo.
Mazishi yakifanyika.
Maafisa Tarafa kutoka Tanga, Singida na mikoa mingine wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la mwenzao Doris.

Baadhi ya Wanahabari wa Mkoa wa Singida wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la mwanahabari mwenzao Doris Meghji.

Baba na Mama wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa mtoto wao Doris Ntaliaga Meghji.


Na Dotto Mwaibale, Singida


SIMANZI, Vilio na Majonzi  vilitawala katika Misa Takatifu ya kumuaga marehemu Mwanabahari Doris Meghji iliyofanyika Kanisa Katoliki Jimbo la Singida.

Akiongoza misa hiyo jana Askofu wa Jimbo Katoliki Singida Mhashamu Edward Mapunda alisema  Kanisa hilo limempoteza mwanahari huyo ambaye alikuwa mtangaji wa Radio Maria ambayo inasimamiwa na kanisa hilo.

" Namfahamu Doris kama mlivyosikia yeye ndiye alikuwa mtangazaji wa kwanza wa Radio Maria tulipotangaza nafasi ya kazi Doris alijitokeza na kuwa mwakilishi wa Radio yetu ,". alisema Askofu Mapunda.

Mapunda alisema walimkubalia kufanya kazi baada ya kujiridhisha kwamba alikuwa ni mwandishi wa habari mzuri na kuwa hata baada ya kupata nafasi hiyo alifanya kazi yake vizuri ya kutangaza neno la Mungu kupitia radio hiyo.

Alisema Doris alitangaza injili kupitia radio hiyo kwa kuwa alikuwa akihifahamu vizuri imani ya Kanisa Katoliki hivyo kutokana na kazi hiyo tunampongeza sana.

Alisema Doris alimuaga kuwa amepata nafasi nyingine ya kazi TBC ambapo alimpa baraka zote ili apate nafasi nyingi zaidi za kulitumikia Taifa baada ya kupata uzoefu mkubwa katika Radio Maria.

Alisema anaamini na  TBC aliwawakilisha vizuri kabla ya kupata nafasi nyingine ya kulitumikia Taifa kwa nafasi ya Afisa Tarafa mkoani Tanga ambayo aliifanya hadi umauti wake."Tuendelee kumuombea kwani kifo cha Doris ni cha baraka, neema na ni mlango wa kuingia mbinguni.. kumuona Mungu," . alisema Askofu Mapunda.

 Wakizungumza wakati waakitoa salamu za rambirambi katika Misa hiyo watu mbalimbali waliokuwa wakimfahami Doris walisema alikuwa mchapa kazi na alimuheshimu kila mtu bila ya kujali jinsia yake, cheo chake na umri wake.

Walisema mkoani Tanga alikokuwa akifanya kazi alichaguliwa kuwa kiongozi wa maafisa Tarafa wote wa mkoa huo hivyo inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa akishirikiana na wenzake vizuri katika kazi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Singida Elisante John alisema chama hicho kimempoteza mwanahabari mahiri licha ya kuwa alikuwa akifanya kazi nyingine ya Afisa Tarafa.

"Doris alikuwa mwenzetu na tulifanya naye kazi vizuri tukiwa wote hapa Singida na mimi ndiye niliyempokea na alikuwa mchapa kazi mzuri,". alisema John.

Marehemu Doris Meghji alizaliwa Septemba 15, 1977 mkoani Tabora wakiwa watoto wa kwanza na pacha wake Dorica Meghji ambaye naye ni marehemu.

Marehemu Doris alipata elimu ya Msingi Shule ya Msingi Utemini na baadae Shule ya Sekondari ya Margaret iliyopo mkoani Kilimanjaro.

Baada ya hapo Marehemu alisoma kidato cha Tano na cha Sita Shule ya St.Joseph iliyopo Arusha na baada ya hapo alijiunga na Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT) jijini Mwanza ambapo alisomea Uandishi wa Habari Ngazi ya Cheti na kuendelea na masomo zaidi ya fani hiyo hadi kupata Shahada.

Enzi za Uhai wake marehemu alifanya kazi sehemu tofauti tofauti kama Sibuka FM, EFM, Gazeti la Tanzania Daima, Mtangazaji wa Radio Maria, TBC, Standard FM, Azam TV na Afisa Tarafa Ngamiani mkoani Tanga.

Mazishi ya Mwanahabari huyo yalihudhuriwa na viongozi kutoka  Serikalini, vyama vya siasa, madiwani, Meya wa Manispaa ya Singida  na wananchi kutoka sehemu mbalimbali wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Singiga mjini Ramadhan Mussa Sima.

Post a Comment

0 Comments