Na Calvin
Gwabara - Dodoma
NAIBU Waziri
wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amewaahidi
wadau wa Kilimo Hai nchini kuwa anakwenda kuanzisha Kitengo maalumu kwenye Wizara
hiyo badala ya dawati lililopo sasa ili kuongeza msukumo utakaosaidia kukua kwa
Kilimo hai ili kuchangia kuleta tija kwa Taifa tofauti na ilivyo sasa.
Kauli hiyo
ameitoa wakati akizfungua Kongamano la pili la kitaifa la Kilimo hai
lililowakutanisha wadau wote kutoka ndani na nje ya Tanzania likijumuisha
Wizara ya Kilimo,Mbalozi wa nchi mbalimbali,Wakulima wa Kilimo hai na
wasndikaji,Mashirika ya Kimataifa,Sekta binafsi,Taasisi mbalimbali za Utafiti
linalofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.
“Najua kuwa
kwa sasa pale wizarani tunalo dawati linaloshughulikia masuala mbalimbali ya
kilimo Hai lakini kwa kutambua umuhimu wa kilimo hiki nawaahidi kuwa nakwenda
kuanzisha Kitengo maalumu na sio dawati tena ambalo nguvu yake inaonekana sio
kubwa na ninamini kupitia kitengo hiki kitasaidia kuweza kufikia malengo
tnayoyakusudia”Alisema Mhe. Bashe.
Naibu Waziri
huyo wa Kilimo amesema duniani kwa sasa watu wamekuwa wanzingatia sana swala la
afya kutokana na vyakula wanavyokula lakini pia mazao yatokanayo na kilimo Hai
yanabei nzuri kuliko yae mengine yasiyo ya kilimo hai hivyo kama wizara lazima
ihamasishe na kuhimiza ukuaji wa Kilimo hai Nchini.
Bashe
amesema pamoja na jitihada hizo ambazo Wizara yake inakwenda kuzichukua lakini
pia kwa kushirikiana na wadau hao amedhamiria kuanzisha benki ya mbegu za asili
nchini ambayo itakuwa na kila aina ya mbegu nzuri ambazo wazee wamekuwa
wakizutumia kwa miaka mingi ambazo zitasafishwa vizuri ili ziweze kurudishwa
mashambani.
“Namuagiza mkurugenzi wa TARI nchini kama
anavyohangaika kufanya tafiti za mbegu,mbolea na madawa sasa nataka awe na
kitengo maalumu cha utafiti ambacho kitakuwa kinashughulika na maswala ya
kilimo hai nchini kwa upana wake” aliagiza Bashe.
Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa TOAM,Dkt. Mwatima
Juma alisema wakati sasa hivi kwenye kongamano hili hawazungumzii tena kuwa na
kilimo hai bali wanazungumzia sasa nini kifanyike maana kuendelea na malumbano
ya kufaa kwa mbolea na chumvichumvi na kutofaa au kuzungumzia dawah ii na ile
ni jambo ambalo halikipeleki mbele kilimo hai nchini .
“Sasa hivi
kote duniani imeshafahamika kwamba matatizo ya tabia nchi,matatizo ya
kiuchumi,matatizo ya ajira yote yanatokana na mfumo usiofaa wa kupeleka mbele
swala zima la kilimo hai kwahiyo tujaribu kuona ni namna gani na kuweka mkakati
wa namna ya kuweka mfumo mwingine” alisisitiza Dkt. Mwatima.
Aliongeza
Hivi sasa mkutano mzima utasikia mamswala ya tumefanikiwa wapi, nini kifanyike
kupanuka zaidi kwa sababu kuna swala zima la utafiti,swala zima la Siasa ambayo
yote yanatakiwa yaende sambamba ili kuona mambo ya kilimo endelevu na kilimo
hai kinapofika.
“Sababu
kubwa ya mimi binafsi ya kutaka tuelekee huko ni sababu ya kiafya kwani afya
zetu zinaharibika sana kutokana na mfumo wa uzalishaji ambao umeharibika
kwahiyo tunauchimbua kutoka kule ili tuweze kurekebisha maswala ya afya ili
kupunguza matumizi ya rasilimali zetu kwenye matibabu, Tuna swala la
mazingira,tuna swala la mabadiliko ya tabia nchi pamoja na swala la uchumi wa
nchi,swala la kupatikana soko kwa mazao yetu,kuongeza thamani ya amzao yetu
ambayo hapo utaona kuna kuongeza ajira kwa vijana” alibanisha Dkt. Mwatima.
Waziri wa Kilimo,Umwagiliaji na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Soud
Hassan alisema hivi sasa karibia asilimia 60 ya mazao ya Zanzibar ni Kilimo Hai
maana walikuwa wakilima hivyo kwa muda mrefu bila kutambua kuwa ni kilimo Hai.
“Kama
mnavyojua kuwa Zazibar tunalima sana viungo na kinawaingizia wakulima wetu
fedha nyingi sana na kusaidia katika uchumi wao na Serikali lakini lazima
tuseme ukweli kuwa kilimo Hai wafadhili wakubwa ni watu kutoka nje lakini
niwahakikishie kuwa nitakaporudi Zanzibar wakati wa bajeti naiweka kilimo hai
kwenye bajeti hiyo kwa lengo la kuendeleza kilimo hiki” alisisitiza Hassan.
Kongamano hilo la pili la Kilimo Hai linafanyika jijini Dodoma likiwa na kauli mbiu isemayo Kuchochea kilimo hai kwa mfumo endelevu ya Chakula.
0 Comments