anayetetea nafasi hiyo asipate upinzani.
Richard Kilumbo
Kikao hicho kilichoketi Septemba 12, mwaka huu katika ofisi za CCM Wilaya kikiwa na wajumbe wanane, Mwenyekiti wa kikao alikuwa ni Richard Kilumbo ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya huku mwandishi wa kikao akiwa ni Mbunge wa Kyela, Ally Mlagila.
Taarifa za ndani kutoka katika kikao hicho ambazo zimelifikia gazeti hili ni kwamba katika wagombea tisa waliochukua fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kyela watatu ndio wamepewa alama B ambao kwa mujibu wa kikao hicho ndio wana sifa.
Waliopewa alama B ni pamoja na Mwenyekiti wa sasa anayetetea nafasi yake Patrick Mwampeta, wengine ni Adelina Kabefu ambaye ni mfanya usafi katika ofisi za halmashauri ya Wilaya Kyela na Benjamin Mwakibunda ambaye ni mjasiliamali.
Hatua ya Kabefu na Mwakibunda kupewa alama B na kupendekezwa na Kamati ya Siasa ya Wilaya kwamba ndio wanaofaa kugombea nafasi hiyo wakati hawajawahi kushika nafasi yeyote ya uongozi ndani ya chama kumezua mjadala mzito ndani ya wanachama wa CCM Wilaya ya Kyela.
Taarifa za ndani zimeelezwa kuwa Kabefu na Mwakibunda wamependekezwa japo hawana sifa na kuwaacha wazoefu katika uongozi ili kumwezesha Mwenyekiti wa sasa wa CCM asipate upinzani wakati wa uchaguzi.
Kutokana na hali hiyo,baadhi ya wagombea wamelazimika kuandika barua kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya kupinga maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Siasa ya Wilaya ambayo imeonyesha dhahili inataka kumbeba Mwenyekiti wa CCM Wilaya anayetetea nafasi hiyo.
"Kikao cha Kamati ya Siasa kimsingi kilikuwa na mizengwe mingi kwanza kila mjumbe anadaiwa kupewa Sh.200,000 ili kukubali maamuzi ya viongozi watakavyoamua," kilisema chanzo cha habari kutoka ndani ya kikao.
0 Comments