Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida Jumanne Ismail Makhanda akiwa amepiga magoti mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ikiwa ni ishara ya kumshukuru baada ya kutoa ahadi ya kupaua ukumbi unaojengwa na chama hicho wilayani humo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoianza Februari, 27, 2023.
Na Dotto Mwaibale, Manyoni
KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo amekuna
nyoyo za wanaccm Wilaya ya Manyoni mkoani Singida baada ya kuahidi kupaua na kuezeka ukumbi wa
ccm wa chama hicho hali iliyomfanya Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Manyoni, Jumanne Ismail Makhanda kupigwa butwaa na kulazimika kumpigia
magoti ikiwa ni ishara ya kumshukuru.
Makhanda alifanya tukio hilo februari
27, 2023 baada ya Chongolo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ukumbi huo
wakati wa siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo
inayofanywa na chama hicho ili kuona utekelezaji wa ilani 2020/ 2025.
Chongolo baada ya kuweka jiwe hilo la msingi aliahidi kutoa mifuko ya
saruji 200 na kuliezeka jengo hilo huku Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter
Serukamba akiahidi kuchangia mifuko 70 na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemilembe
Lwota akiahidi kutoa mifuko 30.
"Ninawapongeza sana Wana CCM wa Manyoni kwa kuwa wabunifu wa miradi na
kuitekeleza vizuri na mimi nawaahidi nitakwenda kuzungumza na Mwenyekiti wa CCM
Taifa, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tuone namna ya kulipaua jengo hili"
alisema Chongolo.
Katika hatua nyingine Chongolo, amewataka vijana kuacha kukaa vijiweni
badala yake waende kujiunga na mafunzo
ya ufundi na kupata ujuzi utakaowawezesha kuwa na kazi za kufanya.
Chongolo aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Chikuyu
wilayani humo baada ya kukagua mradi wa maji wa Kitinku Lusilile utakaogharimu
Sh.bilioni 12 hadi kukamilika ambapo
alisema serikali imetoa fursa kwa vijana kusoma programu za ufundi bure
zinazotolewa kwenye Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA).
Chongolo alisema kumekuwa na changamoto ya vijana wengi hapa nchini
wanapomaliza vyuo akiwa na shahada mfano ya Kiswahili anakuwa na mashaka kama
anaweza kufanya kitu kingine zaidi ya hiyo taaluma aliyonayo.
"Wananchi msiache kupeleka vijana kwenye mafunzo ya ufundi,vinajengwa
vyuo vya VETA nchi nzima lengo ni kusogeza elimu ya ujuzi mahususi karibu na
wananchi hivyo pelekeni vijana wakapate ujuzi kwani itawapa uhakika wa
kujiajiri na kupata shilingi," alisema.
Alisema haipendezi unajengwa mradi sehemu fulani lakini madirisha
yanakwenda kuchomewa wilaya au mkoa mwingine wakati kama vijana wangepelekwa
kwenye mafunzo ya ufundi wangeweza kuzifanya kazi hizo na hivyo kujipatia ajira
na pesa.
"Hakuna mbadala mwingine bila kuandaa watu wetu,tusipoandaa wa kwetu
tutakuja kufanyiwa kazi na wengine, haipendezi tunajenga kituo cha afya hapa
watu wa kuja kupiga bati wanatoka Iringa na siku akija Katibu Mkuu mtasema
unaona hawa ndugu zako, hapana hivi haivutii tuna uwezo kutengeneza watu
wetu," alisema.
Chongolo akizungumza mradi wa maji wa Kitinku Lusilile, alisema kabla
hajaondoka mkoani Singida cheti cha
msamaha wa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambacho kimekwamisha kuanza kwa
mradi huo kinapatikana haraka.
"Hatuwezi kuwa tunajadili vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji fedha
kuvichukulia hatua na kuvitekeleza, hivi inaonyesha kuna watu wapo katikati
hawataki kutimiza wajibu wao na sisi hatupo tayari, tunachotaka ni kupeleka
huduma ya maji kwa wananchi," alisema na kuongeza.
"Tunajadili suala la 'certificate' wakati Wizara ya Maji na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) wote wanatumikia serikali ya CCM iliyo chini ya Rais
Dk.Samia Suluhu Hassan, sasa nataka kabla sijaondoka Singida certificate iwe
imefika," alisema.
Hatua ya Katibu Mkuu wa CCM kutoa agizo kwa mamlaka husika kutoa cheti cha
msamaha wa kodi ilitokana baada ya Meneja wa Wakala wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa
wa Singida, Said Lucas, kueleza kuwa miradi wa maji Kitinku Lusilile umechelewa
kuanza ujenzi awamu ya tatu kutokana na TRA kuchelewa kutoa cheti cha msamaha
wa kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter
Serukamba, alisema kama cheti cha msamaha wa kodi kingekuwa kimetolewa
mkandarasi aliyepewa zabuni ya kujenga mradi huo angekuwa ameanza kazi.
Awali taarifa ya ujenzi wa mradi huo iliyotolewa na Kaimu Meneja wa RUWASA
Wilaya ya Manyoni,Shija Maduhu, alisema mradi huo utakapokamilika Disemba mwaka
huu utahudumia vijiji 11 vyenye zaidi ya wananchi 55,000.
Mradi wa Kintiku Lusilile ambao umeanza kujengwa mwaka 2017 hadi kukamilika
kwake utagharimu Sh.Bilioni 12 ambapo katika awamu ya kwanza serikali ilishatoa
Sh.bilioni 2.8, awamu ya pili Sh.bilioni 3.3 na awamu ya tatu zimetolewa
Sh.bilioni 5.6 ambazo zinasubiri TRA itoe cheti cha msamaha wa kodi VAT ndipo
mkandarasi aendelee na kazi.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Itikadi na Uwenezi, Sophia
Mjema aliwataka Wana CCM kuendelea kuisimamia miradi ya maendeleo
inayotekelezwa katika maeno yao na
kuhakikisha inalingana na fedha zinazotolewa na erikali.
Mwenykii wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata alisema mafanikio makubwa ya utkelezaji wa miadi ya maendeleo mkoani humo yanatokana na ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa chama na Serikali.
Leo februari 28, 2023 Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo anaendelea na ziara katika Wilaya ya Ikungi.
Kijana wa itifaki wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM,) Alex Thomas akimpatia maua Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Mbwasa kilichopo Kata ya Chikuyu wilayani Manyoni kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani Singida. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha MlataKatibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa ukumbi wa CCM Wilaya ya Manyoni..
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Itikadi na Uwenezi, Sophia Mjema, akizungumza katika ziara hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata.Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakionesha furaha baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa fremu za maduka ya chama hicho wilayani Manyoni.Kushoto mwenye kipaza sauti ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniface.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi,Daniel Chongolo akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter (kushoto) wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Solya iliyopo Tarafa ya Kilimatinde, Kata ya Solya, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemilembe Lwota akizungumza kwenyeziara hiyo.
Kikundi cha Wanawake Tawi la Igose- Ngaiti Manyoni kikitoa burudani wakati wa mapokezi hayo.
Mapokezi yakiendelea.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy Boniface akizungumza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo. Kulia kwake ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Singida, Violet Soka.
Wabunge wa Singida wakionesha fuaha yao wakati wa mapokezi hayo. Kutoka kulia ni Mbunge a Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Gwau, Mbungewa Singida Kaskazini, Ramadhan Ighondo, Mbunge wa Singida Mjini,Mussa Sima na Mbunge wa Mkalama, Isack.Francis
Viongozi wa CCM wakionesha furaha zao wakati wa mapokezi ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Muonekano wa mapokezi hayo.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu akiongoza mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Wabunge wa Singida na viongozi wa CCM wakiserebuka wakati wa mapokezi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaa ya Mkalama, James Mkwega muda mfupi baada ya kuwasilikuanza ziara yake ya kikazi mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ikungi, Ahmed Missanga muda mfupi baada ya kuwasilikuanza ziara yake ya kikazi mkoani Singida
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Manyoni,Shija Maduhu, akitoa taarifa ya mradi wa maji Kintiku Lusilile mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo (kushoto)
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (kushoto) akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Muonekano wa jengo la Utawala la Shule ya Sekonari ya Wasichana Mkoa wa Singida inayojengwa Kata ya Solya wilayani Manyoni ambayo ujenzi wake umekaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dk.Pius Chaya akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC) Mkoa wa Singida, Yohana Msita akizungumza kwenye ziara hiyo.
Wananchi wa Wilaya ya Manyoni wakimsubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, akiwatuza wasanii wa kikundi cha utamaduni waliokuwa wakitoa burudani wakati wa ziara yake wilayani Manyoni.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akizungumza kwenye ziara hiyo.
Wakina mama wa CCM wakimpungia mikono Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati alipotembela Shina namba Tano wilayani Manyoni.
0 Comments