Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro, akizungumza wakati akifunga mafunzo ya wahitimu wa dini ya kiislam katika Madrasa ya Siraj i iliyopo Msikiti wa Kibaoni mjini hapa hivi karibuni.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro ameuomba uongozi wa Mkoa wa Singida
kuyatokomeza madanguro na vijiwe vyote vya wanawake wanaojiuza kuhakikisha
vinavunjwa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Nassoro alitoa ombi hilo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo
ya wahitimu wa dini ya kiislam katika Madrasa ya Siraj i iliyopo Msikiti wa
Kibaoni mjini hapa.
"Kwa heshima hii ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani naiomba Serikali ya
Mkoa wa Singida, kuhakikisha madanguro yote yaliyopo mkoani Singida yanatokomezwa"
alisema Nassoro.
Katika hatua nyingine Sheikh Nassoro amewataka waumini wa dini ya Kiislam
mkoani hapa kuacha tabia ya kuwabeza, kuwadhalilisha na kuwashutumu walimu wa
dini badala yake watambue thamani yao.
Alisema waislam wanatakiwa kutambua
kuwa walimu hao sio malaika bali ni wanadamu wanamapungufu kama ilivyo
kwa watu wote na katika mapungufu hayo wachukue yaliyomema kutokana na adhi
yao.
Alisema waimu hao wa dini wanafanya kazi kubwa sana katika madrasa
mbalimbali tena katika hali duni, hawana posho huku mishahara yao ikiwa ni
matusi, kudhalilishwa na kupewa maishaaaaa mabaya.
Sheikh Nassoro aliwaomba waislam kuanzia sasa kujenga utamaduni katika
misikiti kuhakikisha linapatiana fungu la walimu hao wa madrasa.
Aidha, aliwataka walimu hao wa dini kuhakikisha wanasimamia maadili kwa
watoto wa kiislam hasa katika kipindi hiki cha sasa ambapo dunia inawaangaza
watoto wa kiume katika kuleta hadaa ya kuwagiribu ili wawe mabarazuri ;mashoga;
“Sinto pendezewa, sinto furahi, sintosikia amani kusikia moja ya madrasa
kuna watoto ambao ambao wameanza kuwa mabarazuri” alisema Nassoro.
Sheikh Nassoro pia alisema masheikh wa kata ndio wasemaji wa kuu wa
waisalam katika kata zao hivyo
wanatakiwa kuwasemea waislam na kuupigania uislam na si vinginevyo.
Alisema hivi sasa wanaingia katika kipindi cha mafungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani moja ya wajibu wao ni kujua idadi ya waislam waliopo kwenye maeneo
yao hasa watu wenye mahitaji maalumu wakiwepo mayatima jambo litakalosaidia
kuwapatia misaada ya kibinadamu.
Sheikh Nassoro alitumia nafasi hiyo kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwaomba wafanyabiasha wasipandishe bei ya vyakula katika mwezi huu kama alivyofanya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Sheikh wa Kata ya Kibaoni, Ramadhani Shabani akizungumza kwenye hafla hiyo.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro akiteta jambo na Mwalimu wa Dini, Hamisi Ndigha wakati wa hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Ashrafu Amani mmoja wa washindi wa mafunzo hayo akipatiwa zawadi mbalimbali.
Ashrafu Amani mmoja wa washindi wa mafunzo hayo akiwa amebebwa.
Taswira ya hafla hiyo.
Vijana wakicheza qaswida katika hafla hiyo
0 Comments