Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida mjini Mussa Sima ametoa Sh.200,000 kwa ajili ya kusaidia
makundi mbalimbali ya watu wakiwemo yatima, wajane, wazee na wafungwa katika
kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Sima alitoa msaada huo baada ya Ofisi ya Sheikh Mkoa wa Singida kupitia kamati
maalumu ijulikanayo kwa jina la Nusratan al Ummati Singida kumuandikia barua ya
kumuomba kuchangia chochote alichonacho kwa ajili ya makundi hayo.
Kamati hiyo inajishughulisha kutoa huduma kwa wajane, mayatima, wafungwa,
wazee, watu wenye mahitaji maalumu na vyuo mbalimbali.
Katika sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na kamati hiyo iliandikwa
“Tunayofuraha kuwaomba mahitaji haya kwenu kwani tunawahitaji wengi kama
binadamu tunapaswa kupendana, tuhurumiane, tukumbukane na tukumbushane kama Mungu
anavyotuelekeza” ili eleza sehemu ya barua hiyo.
Mahitaji ya kamati hiyo katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu ni kupata
mchele tani 5, sukari tani moja, mafuta lita 1000, maharage tani mbili, viazi
tani mbili na kuwa mtu yeyote atakaye kuwa tayari kuchangia kwa chakula anaweza
kupeleka ofisi ya sheikh wa mkoa na yule ambaye atapenda kutoa fedha anaweza
kuingiza katika akaunti NUSRATUN AL UMMATI Singida namba 01527146400 Bnki ya
CRDB.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Sheikh Mkoa wa Singida, Issa
Nassoro alimshukuru Mbunge Sima na kueleza kuwa watu wengine na wabunge wenzake
nao wanaombwa kusaidia makundi hayo kwa chochote watakacho jaaliwa na Mwenyezi
Mungu kwani kutoa ni moyo na si utajiri.
Kwa mtu yeyote atakayekuwa tayari kuchangia anaweza kuwasiliana na Katibu wa Baraza la Masheikh Mkoa wa Singida kwa namba ya simu 0757713272 au 0713378249.
0 Comments