Na Nyamizi Moses - Tabora
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa
Tabora Hasasn Wakasvi amewakemea vikali watu wanaotumia vibaya majina ya
viongozi wa juu kutafutia kura Kwa lengo kuchaguliwa kwenye chaguzi zijazo
Akizungumza katika karika Sherehe ya uzinduzi wa miaka 47 tangu CCM
kuzaliwa, ambazo zimefanyika kata ya Tura wilaya ya uyui mkoani Tabora,
Wakasuvi amesema kunawatu wamenza kupita Kwa wananchi wakidai CCM imewatuma
kugombea hivyo waungwe mkono wakati wa uchaguzi ujao wa 2025
"Nimepata taarifa huku Jimbo la IGALULA Kuna watu wanapitapita na
kusema kuwa sisi chama tumewatuma eti waje kugombea sisi hatujawatuma kufanya
jambo hilo. Alisema Wakasuvi.
Hata hivyo Wakasuvi ambaye pia ni Mjumbe kamati
kuu ya CCM taifa amebainisha kuwa watu hawazuiliwi kupita kuweka Mambo sawa Kwa
wapiga kura lakini ni vema wakapita kimyakunya bila kufanya vurugu.
Aidha amewataka watu wanaotaka kugombea nafasi za
ubunge, udiwani na wenyeviti wa vijiji kuacha mara Moja kuwachafua wenzao ambao
Bado wapo madarakani kuwa wastarabu Kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kusabanisha
mtafaruku ndani ya chama pia kuleta chuki baina yao.
Wakasuvi amesema kuwa chama Cha mapinduzi hakipo
tayali kuteua mgombea ambaye Hana sifa ya uongozi nakwamba mgombea anaetaka
kugombea KUCHUKUA fom ya kugombea apime na
ahakikishe anazo sifa za kupeperusha vema Bendera na hatimaye kukipatia
ushindi mnono chama Cha mapinduzi na sio vinginevyo.
"CHAMA katika Wilaya zote hapa Tabora hakipo tayali kuteua mtu ambaye haleti maendeleo Kwa jamii" amesema Wakasuvi.
0 Comments