..........................................
Na Hastin Liumba,Tabora
TUNAVYOFAHAMU barabara ni kielelezo na kichocheo
cha ukuaji wa uchumi nchini na fedha nyingi zimekuwa zikitumika kwa ajili ya
ujenzi toka serikalini kuu kwa ajili ya
ujenzi wake sanjari na ujenzi wa Barabara na madaraja.
Hivyo kwa kutambua hilo ndiyo maana serikali
inachukua hatua za makusudi kutenga fedha nyingi kutekeleza miradi ya barabara
mkoani Tabora na kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliopangwa.
Aidha kila mkazi wa mkoa wa Tabora anapaswa kuwa
balozi katika kulinda na kuhifadhi miundombinu ya barabara sanjari na kulinda
madaraja na alama zake.
Mkoa wa Tabora una mtandao wa barabara wenye
jumla ya kilomita 2,188.09 za barabara zinazohudumiwa na wakala wa barabara
(TANROADS).
Kati ya kilomita hizo kilomita 967.09 ni barabara kuu na kilomita 1,158.01 ni barabara za mkoa zikiwemo kilomita 62.99 za wilaya.Wakulima wa wilaya ya Kaliua eneo Ulyankulu wiliovamia mazao mbalimbali kama mpunga na karanga.
Aidha jumla ya kilomita 794.67.49 za barabara kuu ni za kiwango cha lami na kilomita 172.42 ni za changarawe au udongo.
Barabara za mkoa kilomita 53.74 ni za lami na
kilomita 1,104.27 ni za udongo na kilomita 62.99 ni barabara za wilaya
zilizokasimiwa na wakala wa barabara.pia mkoa unahudumia jumla ya madaraja 596
yaliyojengwa kwenye mtandao huo.
Katika kipindi cha mvua hamna sehemu yoyote
isiyopitika kwani barabara zetu zipo kwenye makundi ya hali ya wastani na hali
nzuri oia madaraja yote yapo salama na matengenezo ya barabara yanaendelea
vizuri.
Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Tabora (TANROADS) mhandisi Raphael Mlimaji alisema hayo wakati akiongea na mwandishi wa makala haya ofisini kwake na sehemu ya wilaya za mkoa wa Tabora ambayo zimeathiriwa kiasi na mvua zinazoendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali za mkoa wa huo na wakulima kulima mazao mbalimbali kwenye hifadhi za barabara.
Mkulima wilaya ya Igunga alivyolima kwenye eneo hifadhi ya barabara.
Mhandisi Mlimaji alifafanua kuwa athari zilizopo
kwa baadhi ya maeneo ambazo ni kukatika kwa barabara katika wilaya ya Kaliua na
eneo la Ulyankulu,wilaya ya Sikonge kata Ngoywa,lakini juhudi zinafanyika
kuondoa adha hiyo kwa wakazi wa maeneo hayo ikiwemo kwasihi kuacha kufanya
shughuli za kilimo au ujenzi wa vibanda vya biashara.
Aliongeza kuwa athari nyingine ni wananchi baadhi
ya wilaya kutotii hofadhi za barabara kwa kuendesha kilimo cha mazao mbalimbali
kama mpunga,Karanga,maharage na mahindi kwani hukumu yake ni kifungo miaka 3 au
faini milioni 1.5.
Alifafanua kuwa sheria zipo na zinaelekeza wazi
kwamba kuingia jkwenye hifadhi za barabara kinyume na katazo la sheria ya
barabara namba (29) (1)-(4) na mabadirilo yake ambayo ni sheria unayofanyiwa
mabadieiko inapoonekana na sheria hii ipo tangu mwaka 1932 Kabla ya uhuru wa
nchi hii.
“Wananchi hawa wamekuwa wakikahidi kwani kablya ya kilimo kwanza wamekuwa wakipewa elimu kupitia watendaji wa vijiji na kata wa sehemu husika……..na kama mnavyoona wengine wameziba Kalvati ili kuzuia majiili walime mpunga na tulivyo mashuudas barabara zimekatiaka sehemu mbalimbali za mkoa hii ni hali ya hatari.’alisema.
Sehemu mojawapo iligeuzwa kuwa shamba kwenye hifadhi ya barabara
Mhandisi huyo aliongeza tatizo jingine ni
wananachi kuiba alama za barabarani,kugonga taa,kugonga alama na kingo za
barabara lakini wameendelea kuchukua hatua kwa wahusika kwa wale wote
wanahusika na kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vyombo vya sheria bila
uonevu.
Aliongeza kuwa wilaya ambazo kwa kulima kwenye
hifdhi za barabara ni Igunga,Uyui,Sikonge,Kaliua na ya mwisho ni Nzega.
Mhandisi Mlimaji alisema mazao yanayolimwa kwenye
hifadhi za barabara ni mpunga,karanga,mahindi na maharage ikiwemo alizeti.
Alisema na kwenda mbalimbali kwa kuonyesha kilimo
hicho kupitia kampuni ya (SEED CO) kama mnavyoona kwenye maeneo mbalimbali
katika baadhi ya wilaya.
Alifafanua kuwa hapa kama jinsi tunavyoona athari nyingine ni hawa wafugaji hapa kijiji cha Ibunba wanapitisha mifugo yao katikat ya barabara na hapa athari kuharibika kwa baraba na hata kusababisha ajali kama dereva atakuwa kwenyeSehemu ya barabara iliyoathiriwa na mvua.
Alisema na kusisitiza kuwa sheria za barabarani namba ya mwaka 2007 zinapaswa kufuatwa na alikemea aliwakuta katika wilaya ya Kaliua wakifyatua tofari za saruji kwenye hifadhi ya barabara na wengine kufanya shughuli za kijamii kwa kuweka vibanda vya biashara.
Aidha meneja huyo alitoa maelekezo kwa wananchi
na watumiaji wa barabara hasa wale waliokutwa wakishusha bomba kubwa maji
kwenye hifadhi wakiwa na mitambo na gari kubwa yenye namba za usajili za T 291
DYF chini ya aliyejitambulisha Bhulan Chahuan kama meneja.
Wakulima wakiri kosa.
Kwa upande wao wakulima Mwasiti Hamis na Juma Seleman wa kitongoji wa cha Igambilo waliokutwa wakilima kilimo cha mahindi kwenye hifadhi ya barabara kama shamba darasa (SEED CO) walikiri kosa kwamba alama wanazitambua.
Mkulima Anna Gaspari wa kitongoji cha Nyandweka
wilaya ya Igunga alikiri kosa kwa kusema shamba mpunga analolima kwenye
barabara ni la mume wake na kwamba Bicon waliiona inavyoelekeza ila anaomba
radhi.
Na wakulima wa Kahozia Rashid,Betha Milambo na
Paulo Zengo wa kata ya Pangale walisema Bicon iliypo wanaiona ila hawajui ina
maana gani kwani hawajui kusoma wala kuandika.
Wakuu wa wilaya waongea.
Mkuu wa wilaya ya Sikonge Saimon Chacha alisema
zipo barua zilizotolewa kwa watendaji wa vijiji na kata juu ya madhara ya
kufanya shughuli za kijamii kama kilimo,ufugaji kwenye hifadhi ya barabara.
Chacha aliongeza kuwa bado ipo tabia ya taa za
barabarani,madaraja kama daraja la Mungu na alama za barabara.
Hata hivyo aliwataka wananchi kuwa na subira
kwani zipo athari za utokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa kasi kubwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kaliua Dkt Rashid Chuachua alisema wilaya yake inafanya zake kwa kufuata sheria inavyozingatia na akatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kulima kwenye hifadhi za barabara,kuiba alama za barabarani.
Chuachua alisema na kuonya wale wote wanaofanya shughuli za kijamii au kibinadamu waache mara moja serikali itaanza kuwasaka kuwaafikisha mahakamani.
Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mkondoo kwa nafasi yake alisema anachukizwa na suala kulima kwenye hifadhi ya barabara napenda kusema barabara ni zetu sote kwa kulinda uchumi wetu ambao ndiyo kila kitu tuheshimu sheria.
Picha inavyoonyesha wafugaji wa kijiji cha Ibumba wilaya ya Sikonge wanavyoingiza mifugo yao kwenye barabara Picha zote na Hastin Liumba,Tabora.
0 Comments