TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao
chake cha tarehe 24 Februari, 2024, kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini
Dodoma imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mdogo wa
Udiwani katika kata 23 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 20 Machi, 2024 kwa
asasi za kiraia 11.
Kwa Mujibu wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari
iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima, R. K imeainisha Asasi za kiraia
11 ambazo zimekidhi vigezo na kupewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura
pamoja na kata walizoomba kutoa elimu hiyo kuwa ni Mbogwe Legal Aid
Organization (MBOLAO) Isebya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe,
Sustainable Hub for Policy Initiatives (SHPI) Mshikamano iliyopo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.
Asasi zingine ni Promotion and Women Development
Association (PWDA) Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma/Ujiji, Bagamoyo Community Capacity Empowerment and Education (BCCEE)
Fukayosi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Action for Democratic
Governance (A4DG) Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.
Asasi zingine ni Vanessa Foundation ambayo itatoa
elimu katika kata ya Nkokwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela,
Tanzania Centre for Disability Development Initiatives (TCDDI) Nkokwa iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Safe Society Platform Tanzania (SSPT)
Busegwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama na Isebya iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
Asasi zingine za kiraia zilizopata kibali ni
Youth Against Aids and Poverty Association (YAAPA) ambayo itatoa elmu katika
kata ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji,
Musoma Municipal Paralegal Organisation (MMPO) Mshikamano iliyopo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.
Asasi nyingine iliyopata kibali ni Shirika la
Elimu ya Uraia na Uzalendo “Civic Education and Patriotism Association”
iliyoomba kutoa Elimu katika kata za Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya
Manispaa ya Kigamboni, Msangani iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kibaha,
Fukayosi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlanzi iliyopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Kibata iliyopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kilwa.
Wakati huo huo, Tume pia imetoa kibali kwa asasi
za kiraia tatu ambazo zimekidhi vigezo ili ziweze kutazama uchaguzi mdogo wa
Udiwani katika Kata 23 za Tanzania Bara.
Asasi hizo tatu zitakazoenda kutazama uchaguzi
Mdogo wa udiwani siku ya Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 ni Tanzania Alliance
for Disability Development Initiatives itakayokuwa katika kata ya Mhande
iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Bridge Development Trust
Organisation itakuwa katika kata ya Buzilasoga iliyopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Sengerema na Promotion and Women Development Association itayokuwa
katika Kata ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kigoma/Ujiji.
Aidha, katika kikao hicho, Tume imezitaka asasi
za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura, kuzingatia Mwongozo
wa Elimu ya Mpiga Kura wa Mwaka 2020 katika kipindi chote cha kutoa elimu hiyo
katika uchaguzi mdogo.
0 Comments