RC TABORA AIPONGEZA TPSF KUPELEKA MRADI WA KUPAMBANA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI

Subscribe Us

RC TABORA AIPONGEZA TPSF KUPELEKA MRADI WA KUPAMBANA BIASHARA HARAMU YA WANYAMAPORI


Mkuu wa Mkoa wa Tabora,  Balozi Dkt. Batlida Buriani (katikati) akionesha furaha yake baada ya kufungua semina ya siku mbili ya wadau wa sekta binafsi na umma katika uwekezaji endelevu, kudhibiti biashara ya wanyamapori iliyofanyika mkoani hapa. Kushoto ni  Mratibu Miradi kutoka TPSF, Godfrey Mondy. 
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Nyamizi Moses, Tabora

MKUU wa Mkoa wa Tabora,  Balozi Dkt. Batlida Buriani ameipongeza Taasisi Binafsi ya Uwekezaji Tanzania (TPSF) kwa kuleta mradi wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi mkoani hapa kwani itasaidia na kuendelea kwa uwekezaji pamoja na kupambana na biashara haramu ya wanyamapori.

Balozi Buriani amesema hayo Februari 28, 2024  wakati akifungua semina ya siku mbili ya wadau wa sekta binafsi na umma katika uwekezaji endelevu, kudhibiti biashara ya wanyamapori iliyofanyika mkoani hapa.

Alisema mradi huo  utasaidia kupunguza migongano kati ya binadamu na wanyamapori katika shoroba za Rauha, Rungwa na Inyonga ambayo imekuwepo ikiripotiwa kutolea mara kwa mara hali ambayo  inasababisha kwa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kushindwa kufanya kazi za kimaendeleo.

"Naishukuru TPSF kwa kuja na lengo hili na hatimaye kufika hapa Tabora na kutushirikisha katika mradi huu na tunayo imani kuwa wananchi wa Mkoa wa Tabora watapata fursa na tunaimani uwekezaji utazidi kukua na migogoro itapungua kwa ushirikiano na na mbuga ya Inyonga."alisema Buriani.

Aidha, Dkt Buriani ameitaka taasisi hiyo kuzingatia malengo ambayo imejiwekea na kusaidia wananchi kupata rasilimali mbalimbali kutoka katika maneno ya misitu na shoroba pamoja na kuendelea kupambana na changa moto ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

 "Bila kusimamia mikakati na malengo ambayo nyinyi kama sekta mmejiwekea katika kusaidia jamii itakua ni sawa na bure,hivyo niwasihi sana kusimamia kile mlichopanga na hakikisheni wananchi wanapata rasilimali ambazo zipo katika misitu,kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo tunakosa baadhi ya rasilimali kutoka misituni mfano Mangogoti na Uyoga na hii ni kutokana na ukosekanifu wa utunzwaji wa hivi vitu,hivyo tujitahidi tulinde misitu na tupambane na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi," alisema.

Naye Mratibu Miradi kutoka TPSF ambae pia ni Meneja wa miradi tuhifadhi maliasili ambao umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo Marekani USA, Godfrey Mondy alisema majadiliano yaliyofanyika kati yao na wajasiliamali mkoani hapa yataleta matokeo chanya kwa serikali na wananchi pia itazidi kuukuza mnyororo wa thamani na kuleta fulsa mbalimbali kwa wananchi  mkoani hapa.

"Kupitia mradi huu serikali na wananchi pamoja na nchi kwa jumla itaweza kutambua ni namna gani sekta hii binafsi inaweza kuingia katika ku "support maendeleo ya mnyororo wa thamani na kwa Tabora tumejifunza kuwa kuna kiwanda cha uchakataji wa asali kule Sikonge ambacho kimepatiwa mtu binafsi na inaonyesha ni kwa namna gani serikali ya Tabora inasupport sekta hii,lakini pia tunatoa mafunzo katika kulinda na kuhifadhi maliasili mkoani hapa pamoja na kuleta fursa mkoani Tabora," alisema Mondy.

Hata hivyo, mradi huo wa USA Tuhifadhi maliasili mradi ambao unasimamiwa na Shirika la RTA International kwa kushirikiana na TPSF ni mradi wa miaka 5 ambao ulianza mwaka 2021 na utamaliza  2026 ikiwa na malengo ya kuongeza uwezeshaji kwa maeneo ya private sector ingegment na taasisi za kisheria na taasisi nyinginezo pamoja na kuonyesha sera inayotoa miongozo ya maliasili katika hifadhi ya Aman,Tarangile,Odzungwa, Ruaha Rungwa,  Inyonga na Pwani.Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Post a Comment

0 Comments