Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilida Burian akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa zoezi la kukabidhi vitambulisho vya Taifa zaidi ya 600,000 vilivyotolewa kwa wananchi Februari 14, 2024.
...............................................
Na Nyamizi Moses Tabora
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt Batilida Burian
amekabidhi vitambulisho vya NIDA zaidi ya 600,000 kwa wananchi wa mkoa huo
ikiwa hatua ya kwanza ya ugawaji wa vitambulisho hivyo.
Akikabidhi vitambulisho hivyo mjini Tabora katika
hafla fupi ilifanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Tabora, Dkt Burian amesema hatua hiyo ya Serikali ya
kugawa vitambulisho Kwa wananchi,
itasaidia kuodoa usumbufu kwao wa kukosa namba ya NIDA au kitambulisho
pindi vinapohitajika katika taasisi mbalimbali Kwa ajili kutatua matatizo yao.
Alisema jumla ya vitambulisho vipatavyo milioni 6
na laki 8 vimeletwa mkoani Tabora ili vigawiwe Kwa wananchi ambao
walijiandikisha kupata vitambulisho hivyo tangu zoezi la vitambulisho kuanza
hapa nchini.
"Nichukue fursa hii kuishukuru Serikali
ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia kwa kuleta vitambulisho hivi Kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora, kwani
itakuwa ni mwarobaini wa kutatua kero Kwa wakazi wa mkoa wa Tabora, alisema Dkt
Burian.
Aidha amesema kuwa malalamiko mengi ya wananchi
yalikuwa ni kukosekana kwa vitambulisho vya Taifa (NIDA) hali ambayo ilikuwa ikileta
mahusiano mabaya kati ya Serikali na wananchi wake na kuona Serikali imeshindwa
kutatua kero hiyo.
Amesema kwamba hali hiyo, pia ilipelekea wananchi wengi kukosa huduma
muhimu mbalimbali ikiwemo kusajili laini za simu, kufungua akaunto benki na
hata kumwekea mtu dhamani ndugu pindi vinapohitajika.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi hao ambao
walikabidhiwa vitambulisho vyao ni pamoja na Thomas Shija na Josephina Benedict, ambao wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea vitambulisho vyao kwani awali walikuwa
wakipata tabu sana katika shuguli zao hasa wakati wa kutatua matatizo yao, huku Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Tabora Iddi Mambo akisema CCM
itaendelea kutekeleza kwa vitendo ilani yake ya uchaguzi kwa kutatua kero za
wananchi.
Alisema CCM Mkoa wa Tabora itahakikisha kwamba kero mbalimbali za wananchi zinapungua hasa kwa kuendelea kuisukuma Serikali kuongeza kasi katika upatikanaji wa vitambusho vya NIDA na namba za NIDA kwa wakati.
0 Comments