SPIKA DKT. TULIA AFUNGA MKUTANO WA IPU MAREKANI

Subscribe Us

SPIKA DKT. TULIA AFUNGA MKUTANO WA IPU MAREKANI

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisaini Kitabu cha Maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob, katika Ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo uliopo New York nchini Marekani leo tarehe 9 Februari, 2024. Mhe. Geingob alifariki dunia tarehe 4 Februari, 2024 katika Hospitali ya Lady Pohamba Jijini Windhoek alikokuwa anapatiwa matibabu ya saratani.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akihitimisha Mkutano wa Kibunge wa IPU kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa uliofanyika tarehe 8 na 9 Februari 2024, New York nchini Marekani leo tarehe 10 Februari, 2024. (Kushoto ni Katibu Mkuu wa IPU Ndg. Martin Chungong na kulia ni Patricia Torsney - Msimamizi wa Ofisi ya Kudumu ya Uangalizi ya IPU kwenye Umoja wa Mataifa)
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akichangia mada wakati wa Mkutano wa Kibunge wa IPU kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani leo tarehe 9 Februari, 2024. Mkutano huo uliodumu kwa siku mbili, ulifikia maazimio mbalimabli yakiwamo ya kuhakikisha Mabunge yanakuwa chachu ya kuleta na kudumisha amani duniani, kutumia ukuaji wa akili bandia katika kulinda amani na Usalama Duniani pamoja na kuchagiza uwazi na kuongeza juhudi za kuzisimamia Serikali za Mabunge Wanachana kufikia malengo ya kujenga kuaminiwa na Wananchi wao. 
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi Rais wa Club de Madrid, Mhe. Danilo Turk, zawadi ya ngao kutoka IPU katika Ofisi ndogo za IPU zilizopo New York nchini Marekani tarehe 8 Februari, 2024.

Post a Comment

0 Comments