...................................
Na Issa Mwadangala, Polisi Songwe.
WAANDISHI wa Habari wa Mkoa wa Songwe wamempongeza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Theopista Mallya kwa kupandishwa cheo kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi na kuwa SACP.
Akizungumza baada ya kutoa cheti cha pongeza kwa kamanda huyo Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Songwe, Stephano Simbeye alisema uamuzi wa kumpongeza Kamanda Mallya ni matokeo ya makongamano ya majadiliano yaliyofanyika mwaka Jana baina ya Polisi na waandishi wa habari.
“Tumeamua kuja hapa kwako Kamanda Ili tukupongeze kufuatia kupandishwa cheo na kuwa tunaamini haya ni mafanikio yako binafsi lakini pia inatokana na ushirikiano wa wananchi wote wa Songwe," alisema Simbeye.
Akizungumza baada ya kupongezwa Kamanda Mallya amewataka waandishi wa habari mkoani hapa kuendelea kuielimisha jamii dhidi ya kupinga vitendo vyote vya ukatili.
Alisema pamoja na kupongezwa kwa hatua ya kupandishwa cheo, lakini si mafanikio yake, bali inatokana na kazi nzuri iliyofanywa na vyombo vya habari kutangaza wakati akitoa elimu kwa jamii kuhusu ukatili.
“Vitendo vya ukatili kwa ujumla wake ni vitendo vibaya ambavyo vinasababisha wanaofanyiwa kuamua kujiua, unakuta mtoto mdogo anafanya maamuzi kama hayo ambayo ukifuatilia nyuma yake kuna ukatili uliofanyika,” alisema SACP. Mallya.
Ameongeza kuwa vyombo vya habari viendelee kutoa elimu kwa jamii kuhusu ukatili na mwisho wa siku watu wote wataelimika na kuacha ukatili.Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Songwe wakiwa ofisini kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo kabla ya kumkabidhi cheti cha kumpongeza kwa kupandishwa cheo.
0 Comments