“Mkamate huyo bwana
sasa hivi aende polisi akafunguliwe mashtaka, huyu ni wa kupeleka mahakamani
moja kwa moja. DPP aelezwe afungue jalada la mashtaka. Wale wenzake
tumewapeleka mahakamani tayari sababu tulibaini walihusika na wizi kama huu
kwenye Manispaa ya Kigoma mwaka jana.”
Ametoa agizo hilo leo
jioni (Jumanne, Februari 27, 2024) wakati akizungumza na madiwani na watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwenye kikao kilichofanyika katika kwenye
Halmashauri hiyo, mkoani Mara.
Waziri Mkuu amefikia
hatua hiyo baada ya kuwaeleza watumishi na madiwani mbinu wanazotumia watumishi
wachache wa baadhi ya Halmashauri ambao walikuwa wanashirikiana na watumishi
watatu wa kitengo cha Treasury Single Account (TSA) kuiba fedha za umma.
Akitolea mfano juu ya
mbinu zinazotumika na wachache hao, Waziri Mkuu aliwaeleza watumishi wa
Halmashauri hiyo pamoja na Madiwani kwamba Juni 10, 2023 walitumia mwanya wa
kuombea kibali fedha za bakaa kwa barua iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji, Bw. Chatta Luleka, kwenda HAZINA.
“Ilipofika Juni 30,
walikuwa wamemaliza kutumia fedha hizo na ikabakia sh.milioni 9 lakini kwa kuwa
walishaandika barua ya kuomba kibali, bado fedha hizo zilihamishwa na kuingizwa
kwenye akaunti ya Halmashauri tarehe 19 Juni 2023 na aliyejua alikuwa Bw.
Ishabailu peke yake. Hakutoa tarifa kwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wala wakuu wa
idara.”
“Nilituma timu yangu
hapa ije kufanya uchunguzi, ikawahoji baadhi ya watumishi akiwemo Afisa Mipango
wa Halmashauri, Bw. Wilfred Mwita ambaye alisema hajui uwepo wa hizo fedha wala
hawakuwa na mpango wala bajeti inayohitaji hizo fedha. Mkurugenzi wa sasa, Bw.
Furaha alipoulizwa naye alisema hajui uwepo wa hizo fedha, kwani alianza kazi
Agosti, mwaka jana.”
Amesema Juni 21, mwaka
jana Bw. Ishabailu alianza kufanya matumizi ya hizo fedha kwa kushirikiana na
mfanyabiashara wa hapa Mugumu, Bw. Daudi Matinde Chacha kupitia kwenye akaunti
zake za NMB na CRDB kwa kupitia miamala minne ya sh. milioni 76.3, sh. milioni
57.7, sh. milioni 47 na sh.milioni 32.5.
Amesema alipoulizwa na
timu ya uchunguzi Bw. Matinde alikiri kuwa haidai fedha yoyote Halmashauri ya
Serengeti isipokuwa Mweka Hazina huyo aliomba apitishie fedha zake kwenye
akaunti zake kwa sababu zinahitajika haraka kwa matumizi ya ofisi.
“Aliambiwa atoe shilingi milioni 189 akamkabidhi zote Bw. Ishabailu na
zilizobakia (sh. milioni 24) akaambiwa abaki nazo,” amesema Waziri Mkuu.
“Baada ya kupokea
fedha hizo, Bw. Ishabailu alipanda basi kutoka Serengeti hadi Kituo cha Mabasi
cha Nyegezi, Mwanza na kumkabidhi Bw. Zablon Mponzi ambaye alisema zinatakiwa
haraka na wakubwa huko Dodoma bila kuwataja wakubwa hao ni akina nani. Yeye pia
alikabidhi shilingi 150 kwa huyo Zablon, ina maana alibakia na sh. milioni
39.”
Aliwasisitiza madiwani
na watumishi wawe makini na matumizi ya fedha za umma kwani Mheshimiwa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan anapotafuta hizi fedha na kuzileta kwenye Halmashauri
anataka zije kutatua kero za wananchi walio wengi.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Tarime.
0 Comments