............................................
Na Nyamizi Moses, Tabora
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameongoza mamia
ya waombolezaji na viongozi mbalimbali mkoani Tabora katika mazishi ya aliekua
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu
CCM Taifa Mzee Hassain Wakasuvi ambaye amezikwa leo Februari 24, 2024 nyumbani
kwake Kata ya Mabama wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katika hotuba yake Majaliwa aliwataka wana CCM na Wananchi wa Mkoa wa Tabora kuyaenzi yale yote mema aliyoyafanya Mzee Wakasuvi
na kuishi kwa upendo.
"Mimi niliwahi kuishi na mzee wakasuvi kwa Muda wa miaka minne
wakati huo nikiwa kama Mkuu wa wilaya ya urambo,kiukweli ni mzee ambae alikua
mwalimu wa siasa kwangu,alikua mtumishi mwema katika kazi yake na hakua na
tamaa wala kubagua mtu hivyo niwasihi ndugu zangu tuyaenzi yale yote mema
Ambayo ametuachia mzee wetu" alisema Majaliwa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu (MNEC)
Mkoa wa Tabora ,Hemed Nassoro Hamdan alisema CCM italinda na kuheshimu yale
yote aliyoyafanya wakasuvi kipindi cha uhai wake na kuwataka wanachama kufuata
nyayo za Wakasuvi.
"sisi kama viongozi wa mkoa tuliobaki tutayaenzi na kuyatunza yale
Ambayo mzee wetu aliyapenda na tutahakikisha tunafuata nyayo zake,kwa upendo na
mshikamano,na niwahakikishie ndugu zangu Ccm itajitahidi tupate Tena mtu mwenye
ufanyaji kazi na mshupavu kama Marehemu mzee wetu Wakasuvi,hivyo Tujitahidi
kuwa watulivu kwa sasa na kushikamana". alisema Hamdan.
Nao viongozi wa dini mkoani hapa Askofu Kisiri
Laizer na Sheikh Mavumbi wamesema marehemu ameacha pengo kubwa kwao kwani
alikua ni mtu wa kujitoa katika masuala ya dini na pia alikua ni mtu mwenye
ukweli na msimamo katika dini na hakuwahi kubagua dini yoyote.
Marehemu mzee Wakasuvi alifariki dunia fEBRUARI 22, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete wakati akipatiwa matibabu baada ya kuumwa shinikizo la damu.
0 Comments