Katibu wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Manispaa ya Singida, Hawa Ntandu (kushoto) akimsaidia Mwenyekiti wa Smaujata Mkoa wa Singida, Ambwene Kajula wakati akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa kaka yake David Stephen Kajula aliyefariki Machi 28, 2024 na kuzikwa Machi 31, 2024 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
................................
Na Dotto Mwaibale, (Singidani Blog)
MCHUNGAJI Charles Masunya wa Kanisa la Waadiventista Wasabato la Mwembechai
jijini Dar es Salaam amesema uwepo wa makanisa, Misikiti na Mahekalu mengi
hayajasadidia kuondoa uovu wa binadamu.
Masunya aliyasema hayo wakati akihubiri kwenye ibada maalumu ya kuuaga
mwili wa Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) David Kajula
ambaye alifariki Machi 28, 2024 katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya
ugonjwa wa figo.
"Zamani makanisa yalikuwa machache sana nawalioenda kanisani walikuwa
wachache na uovu ulikuwa mchache lakini leo makanisa ni mengi, misikiti na
mahekalu pia ni mengi sana, angalia kama hili kanisa letu ni kubwa sana lina
eneo la chini na juu (ghorofa) na linaweza kuingiza watu hadi 2000, nenda
katika mikusanyiko utakuta mamilioni ya wakristo, waislamu na watu wengine wa
kila ya imani lakini wingi wao haujaondoa uovu na makanisa yamekuwa ni zizi la
watenda dhambi," alisema Masunya.
Mchungaji Masunya akisoma neno la Mungu kutoka kitabu cha ufunuo sura ya 21
alisema anayefutwa machozi sio kufufuka kwa ndugu zetu bali ni Mungu hivyo ile
dhana ya uwepo wa ndugu zetu mbinguni ambao watawafuta machozi haipo.
Alisema ni vizuri kufarijiana kama wanavyofanya katika tukio hilo la ibada
ya mpendwa wao David Kajula huku wakiamini ipo siku watakuja kukutana na marehemu mbinguni lakini ukweli ni kwmba tukio hilo haliwezi
kubadilisha historia ya marehemu kwa kile alichokiandika kwenye mtihani wake
iwe kwa maombi, kuletwa kanisani na
kupelekwa kaburini kwani alisimama kwa upande wake na iwapo alisimama upande wa
Mungu atapokelewa na Mungu na kama hakusimama upande wa Mungu basi historia na
mtihani wake umekwisha fungwa.
Masunya aliwataka watu wote waliokuwa kwenye ibada hiyo na maeneo mengine kujiandaa kwa
kutenda mema mbele za Mungu katika siku zote za maisha yao hapa duniani ili
mwisho wa maisha yao uwe mwema.
Kwa upande wake Mchungaji Moses Nyange wa kanisa hilo Usharika wa Kiharaka alisema kifo hakivumiliki kwani vyombo mbalimbali duniani vimeweza kuzuia vita na kupata afya njema lakini wameshindwa kuzuia kifo hivyo kila mtu anawajibu wa kuyaandaa maisha yake kupitia imani yake
Mzee Simon Nicholau akizungmza kwa niaba ya familia ya Kajula kwanza kabisa alielekeza shukurani zake kwa Mungu ambaye amekuwa akitupa uhai kwa kuzingatia kuwa duniani watu wote ni wasafiri na kuwahimiza kufunga mikanda na pale anapoona wakikahidi basi ushika breki kidogo kwa lengo la kuwakumbusha.
"Napenda kutoa shukrani kwa kanisa hili kwani mmekuwa wakati ule wa
msiba wa Mama Kajula na Mzee Stephen
Kajula pia tunatoa shukrani zetu kwa kila mmoja wenu aliyefika kutufariji pale
nyumbani Kijichi hadi leo hii ni Mungu tu ndiye atakaye walipa," alisem
Mzee Nicholau.
Katika mazishi ya David Kajula
yalihudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki wakiwepo Mashujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) kutoka Mkoa wa
Singida ambao walifika kumpa pole dada
yake marehemu, Ambwene Kajula ambaye ni Mwenyekiti wa Smujata Mkoa wa Singida.
Waliowawakisha Smaujata kutoka Singida ni Katibu wa Smujata wa mkoa huo,
Juma Maftah na Katibu wa Smaujata Manispaa ya Singida, Hawa Ntandu.
Marehemu David Kajula ameacha watoto wawili wa kike ambao ni Joyce na Ambwene na amezikwa makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Mchi 31, 2024.
Mchungaji Charles Masunya akihubiri wakati wa ibada hiyo.
Mwakilishi wa familia ya Kajula Mzee Simon Nicholau akitoa neno la shukrani.
Mchungaji Moses Nyange kutoka Kanisa la Waadiventista Wasabato Usharika wa Kiharaka akiongoza ibada ya maziko.
Mzee Solomon Mtae ambaye ni Familia Friend na ya Mzee Stephen Kajula akiomba sala ya ya kuhitimisha ibada hiyo ya maziko.
Wanafamilia wakiwa kwenye ibada hiyo.
Heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu zikitolewa.
Mtoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuuaga mwili wa baba yao.
Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuuaga mwili wa baba yao.
David Kajula enzi za uhai wake |
0 Comments