Na Issa Mwadangala, Polisi Songwe
MKUU wa Polisi Kata ya Kalembo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Raphael Magoma
ametoa elimu ya umuhimu wa kunawa mikono kabla na baada ya kula kwa wanafunzi
wa Shule ya Msingi Kalembo iliyopo Wilayani Ileje mkoani Songwe.
Akitoa elimu hiyo Machi 22, 2024 Magoma alielezea umuhimu wa kunawa mikono
kwa wanafunzi hao kabla ya kula na baada ya kula jambo ambalo litawasaidia kwa
afya yao na kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama kuhara na kutapika ambayo
mara nyingi yanasababishwa na uchafu.
Aidha, Magoma aliwataka wanafunzi hao kutumia muda mwingi kujifunza ili
kuongeza maarifa ambayo ni sehemu kubwa ya mafanikio katika maisha yao ya sasa
na baadae.
" Niwaombe walimu muendelee kuwajengea uwezo wa kujieleza wanafunzi hawa mbele ya watu ili waweze kuwa na uwezo wa kujiamini wakati wa kujibu maswali," alisema Magoma.
0 Comments