Wananchi wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wakipita kwenye kivuko cha muda wakiwa wamesongamana. Fedha za ujenzi wa kivuko hicho zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya cha awali kuharibiwa na mafuriko.
.......................................
Na Dotto Mwaibale. (Singidani Blog)
WANANCHI wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamemshukuru Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya kujenga kivuko cha muda baada ya
kukumbwa na mafuriko yaliyoharibu miundombinu ya barabara na madaraja.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao walitoa shukurani za kipee
kwa Rais Dkt. Samia kwa kuwathamini na kutoa fedha za dharura kwa ajili ya
kujenga kivuko hicho wakati wa kisubiri kujengewa cha kudumu.
"Shukurani za pekee zimuendee Mheshimiwa Mama yetu Kipenzi Rais Samia
kwa kututhamni na kutupatia fedha za dharura kwa ajili ya kujenga kivuko cha
muda ili kurahisisha mawasiliano ya usafiri baada ya miundombinu ya madaraja
kuharibiwa na mafuriko," alisema Ramadhani Juma.
Kwa upande wake Hebron Mpangile akizungumzia Kivuko cha Nyameni Ulaya
alisema matumizi yake ni makubwa kwani hivi sasa kuna foleni kubwa ya watu
hivyo ni vema Serikali ikaongeza kasi na
nguvu ya kujenga kivuko cha kudumu.
Mpangile alitumia nafasi hiyo kumpongeza mkuu wa wilaya hiyo , Shaka Hamdu
Shaka kwa uchapakazi wake uliotukuka na kusimamia shughuli za maendeleo huku
akifika kwa wakati kwenye matukio ya dharura kuwaona wananchi na kuchukua hatua
za kuwasaidia jambo ambalo linawatia moyo.
"Huyu mkuu wa wilaya ni wa aina
yake amekuwa akifika kwa wakati kwenye matukio ya dharura na kututia moyo kuwa
Rais wetu hawezi kutuacha yupo pamoja na sisi na kweli tumeziona hatua ambazo
amezichukua za kutusaidia," alisema Agnes Brayson.
Aidha, Brayson alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo, Denis Londo, Diwani, Afisa
Tarafa na viongozi wengine wote kwa jitihada zao wanazozifanya za kuwaletea
maendeleo wananchi wao ikiwa ni kumuunga mkono Rais Samia.
"Kwa kazi hii kubwa mnayoifanya hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwapa
kura nyingi za kutosha mwakani wakati wa uchaguzi mkuu kuanzia za Rais, Mbunge
na Diwani kupitia chama chetu cha CCM," alisema Brayson.
Naye Fadhil Kindamba alisema kabla ya kivuko hicho cha muda ambacho wamepokea fedha za dharura kwa ajili ya ujenzi wake mawasiliano ya vijiji vitatu vyenye zaidi ya wakazi 7000 yalikatika lakini kwa jitihada za viongozi wa wilaya hiyo kupitia Rais Dkt. Samia wamefanikiwa kuyarudisha, hakika Mwenyezi Mungu awatunze na kuwapa afya njema na maisha marefu ili waendeleekuwatumikia.
Wananchi wakipita kwenye maji kabla ya kivuko hicho cha muda kujengwa.
0 Comments