" />

HABARI ZA HIVI PUNDE

MSD KANDA YA TABORA YAONGEZA UPATIKANAJI DAWA, VIFAA TIBA VITUO VYA AFYA


Kaimu Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD),  Kanda ya Tabora,  Adoniezenek Mugisha alizungumzia mafanikio ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya MSD wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria yaliyofanyika kitaifa Mkoa wa Tabora.

......................

Na Mwandishi Wetu, Tabora

BOHARI ya Dawa (MSD) Kanda ya Tabora inayohudumia mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi imeongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba mkoani Tabora katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya tatu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani.

Kaimu Meneja wa MSD,  Kanda ya Tabora Adoniezenek Mugisha amebainisha hayo wakati wa  Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Tabora.

Mugisha alisema MSD Kanda ya Magharibi imeweza kufikisha asilimia 57 hadi 84 ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya Afya vilivyopo mkoani humo.

"Haya ni mafanikio makubwa mno kwetu kwani hapo awali mzunguko wa usambazaji wa dawa ulikuwa ukifanyika mara nne kwa mwaka lakini hivi sasa ni mara sita ndani ya miezi hiyo," alisema Mugisha.

Alisema pamoja na mafanikio hayo changamoto kubwa iliyopo ni miundombinu ya barabara kuwa mibovu na hapa ninapozungumza na ninyi magari yetu matatu yakiwa na shehena ya dawa na vifaa tiba yaliyokuwa yakipeleka dawa Zahanati ya Malolo iliyopo hapa hapa Manispaa ya Tabora yamekwama.

"Changamoto kubwa ya usambazaji wa bidhaa zetu hizi ipo Mkoa wa Kigoma ambapo kuna vituo saba  vya afya ambavyo ili uvifikie ni lazima utumie boti kwani vingi vipo kwenye maji," alisema Mugisha.

Mugisha alitaja changamoto nyingine kuwa ni kutokuwepo kwa mshitiri wa kutengeneza magari yao maalumu kwa kazi hiyo na nitofauti na magari mengine yaliyozoeleka.

Aidha, Mugisha amewataka wananchi kuwa na matumizi sahihi ya vyandarua kama ilivyo tango la kuwakinga na ugonjwa wa malaria badala ya kutumia kwa mambo yasiyokusudiwa.

Katika hatua nyingine Mugisha amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia dawa bila kupima na kupata ushauri wa daktari iii kuepuka kutumia dawa zisizo sahihi ambazo zinaweza kuwasababishia madhara.

Wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Vyandarua vikikabidhiwa wakati wa maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
Maadhimisho hayo yakiendelea.


No comments