………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa
Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson amesema Shirika lolote lisilo la Kiserikali
(NGOs) Mkoa wa Singida litakalo kwenda kinyume na malengo yake ya uanzishwaji
litachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufutiwa usajili wake.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendegu ambaye alikuwa mgeni rasmi
kwenye Jukwaa la Mashirika Yasio ya Kiserikali
(NGOs) mkoani hapa, Apson alisema Serikali aitalivumilia shirika lolote litakalo kwenda kinyume na malengo yake
yaliyomo kwenye nyaraka za usajili.
Mkuu huyo wa
wilaya alisema lengo la jukwaa hilo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu uratibu
na usimamizi wa mashirika hayo na kujadili mchango wake katika maendeleo ya
taifa.
Apson
alitaja malengo mengine ya jukwaa hilo ni pamoja na kuimalisha uhusiano baina
ya Serikali na mashirika hayo kama kauli mbiu ya jukwaa hilo inavyosema “
Mashirika yasio kuwa ya kiserikali ni mdau muhimu, washirikishwe kuhimarisha
utawala bora”
DC Apson
alisema mashirika hayo ni wadau wa Serikali na yanatambulika kutokana na kazi
nzuri yanazozifanya labda tu atokee mtu asieyaelewa na kusema hazioni kazi
zinazofanywa na mashirika hayo.
Mdau wa jukwaa hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Sustainable Environment Management Action - SEMA lenye makao yake makuu mkoani Singida, Ivo Manyaku alisema mashirika hayo yanatakiwa kila baada ya miezi mitatu kutoa taarifa ya utendaji wa kazi zao kwani ni takwa la kisheria.
“Jamani sisi
kama wana sekta tujitahidi sana kutoa taarifa ya kile ambacho tunakifanya,”
alisema Manyaku.
Manyaku
alisema kwa kufanya hivyo itaonesha uhai wa shirika husika kwa kile
inachokifanya na si vinginevyo.
“Inawezekana
ukawa huna mfadhili wala bajeti lakini ukawa unafanya shughuli kama za msaada
wa kisheria uhitaji hata bajeti lakini unazifanya katoe taarifa kuwa
umezifanya,” alisisitiza Manyaku.
Aidha, Manyaku alisema katika taarifa yao inaonesha wamechangia Sh. Bilioni 14.7 lakini walipo zichambua inaonekana ni NGOs nne tu zilizochangia hivyo wanapaswa kuangalia mambo kadhaa kama takwimu, idadi ya wanufaika waliowafikia ikiwemo taarifa zao za fedha.
Manyaku aliongeza kuwa kupitia fedha hizo zilizotajwa hapo juu Sh. Bilioni 14.7 miradi mbalimbali imetekelezwa kwa mwaka 2023/ 2024 mkoani Singida na kuwanufaisha jumla ya wananchi 1, 104, 432 sawa na asilimia 55 ya idadi ya watu waliopo Mkoa wa Singida kwa sensa ya mwaka 2022.
" Huu ni mchango mkubwa katika kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Singida na kama NGOs tunajivunia kwa kuwa sehemu muhimu ya kuchangia maendeleo ya mkoa wetu," aliseama Manyaku.
Mdau wa jukwaa hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Sustainable Environment Management Action - SEMA lenye makao yake makuu mkoani Singida, Ivo Manyaku, akizungumza.Mwakilishi wa Baraza la Mashirika Yasiokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO) Mkoa wa Singida, Happy Francis akizungumza kwenye jukwaa hilo.
Mwezeshaji Onesmo Mdegela kutoka Taassi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida , akitoa mada kuhusu rushwa kwenye uchaguzi.Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Dar es Salaam, Alex Mwambenja akitoa mada kuhusu uzingatiaji wa ulipaji kodi.Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida Dkt. Patrick Kasango, akichangia jambo kwenye jukwaa hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la IMBPD, Hadija Kaherewa (kulia) akiwa na baadhi ya washiriki kutoka makundi maalumu katika jukwaa hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Health Action Association, Selemani Daud, akichangia jambo kwenye jukwaa hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la UTUWANGU Organization, Fatuma Mgeni akizungumza kwenye jukwaa hilo.
0 Comments