Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, akiongoza moja ya Baraza la Madiwani Manispaa ya Singida.
..................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
MANISPAA ya Singida ni moja ya mji ambao unakua
kwa kasi na hali hiyo inatokana na uongozi thabiti wa viongozi ambao
wameweza kuiongoza manispaa hiyo.
Mwanamama Yagi Kiaratu ndiye Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Singida anayeubadilisha mji wa Singida kwa kasi kubwa
akishirikiana na madiwani, mkurugenzi, mkuu wa wilaya na wananchi.
Kwa mtu yeyote anayeishi Singida anaweza kuwa
shahidi wa kasi ya maendeleo yanayoonekana katika mji wa Singida chini ya
Mstahiki meya huyo kuanzia sekta ya afya, elimu, maji, mazingira, miundombinu ya barabara, nishati ya umeme na mengineyo.
Mbali ya kazi hiyo kubwa anayoifanya ni meya wa kwanza mwanamke kushika wadhifa huo katika manispaa ya Singida na amekuwa kiunganishi kikubwa cha wanawake wa Mkoa wa Singida kwa kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo kwenye taasisi za fedha na kuanzisha shughuli za ujasiriamali ili kujiinua kiuchumi.
Aidha, amekuwa akiwahimiza wanawake wa manispaa hiyo kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais utakaofanyika mwakani.
Kupitia nafasi yake hiyo, Kiaratu ameanzisha
utaratibu mzuri wa kusimamia mapato ambapo timu ya madiwani imeundwa kwa ajili ya ufuatiliaji
wa mapato lengo likiwa ni kuhakikisha mianya ya upotevu wa mapato inazibwa.
Baadhi ya mambo yaliyofanywa na Kiaratu ni ununuzi wa magari mapya ya kusomba takataka sehemu mbalimbali za Manispaa ya Singida, kushiriki shughuli za kitaifa zinazofanyika ndani ya manispaa na nje kama mikutano inayohusisha majiji, maonesho ya kilimo, mbio za Mwenge wa Uhuru nk.
Kupitia uongozi wake, Kiaratu amekuwa akitoa nafasi kwa kila diwani kuchangia bila upendeleo jambo linalowafanya madiwani kuwa wamoja na kuiletea maendeleo Manispaa ya Singida.
0 Comments