.....................................
Na Khadija Kalili Michuzi Tv
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamesaidia
kuokoa kiasi cha Bil.1 ,688,289,634.09 katika kipindi cha Aprili hadi Juni
mwaka huu.
Yamesemwa hayo leo Agosti 13 na Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani
Ally Sadiki amesema TAKUKURU ilifanya uzuiaji katika ukusanyaji wa mapato
upande wa ushuru wa huduma katika Halmashauri ya Mji Kibaha na kufanikiwa
kukusanya kiasi hicho cha fedha ambazo awali zilikua zinapotea kwa baadhi kwa
baadhi ya watumishi kushindwa kufuata sheria,kanuni na utaratibu za ukusanywaji
wa mapato upande wa ushuru wa huduma.
"Katika ufuatiliaji huo TAKUKURU imebaini kuwa baadhi ya watumishi wa
Halmashauri Kitengo cha ukusanyaji wa mapato kuwa kuwa na via sheria vya
uvunjifu wa maadili kwa kushindwa kuwajibika katika ufuatiliaji nanukusanyaji
wa ushuru wa huduma.
Amesema kuwa baadhi ya watumishi kuingia makubaliano na wafanyakazi katika
kulipa ushuru wa huduma na kuwaruhusu kulipa kiasi kidogo ukilinganisha na
mauzo yao halisi.
Baadhi ya Wafanyabiashara wanapotaka kulipa ushuru wa huduma wanajikadiria
mauzo yao hivyo kusababisha kulipa ushuru wa huduma kiasi kidogo ukilinganisha
na mauzo halisi kutoka kwenye Z-REPORT kama sheria inavyowataka kutumia
Z-REPORT katika kukokotoa mauzo"amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Sadiki.
Amefafanua kwa kusema kuwq baadhi ya Wafanyabiashara kulipa nusu au
hawalipi kabisa ushuru wa huduma kwa madai kwamba Kibaha ni eneo la uzalishaji
(Viwanda) na siyo eneo la mauzo (Sokoni), hii ni kutokana na wafanyakazi
kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na malipo ya ushuru wa huduma huku
baadhi ya Wafanyabiashara wamegundulika kuwa wanamiliki mashine za EFD zaidi ya
moja hivyo kuficha zingine ili kukwepa kulipa kiasi sahihi anachotakiwa
kukilipa.
Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki ameongeza kwa kusema kuwa
taasisi hiyo imesaidia kuongeza makusanyo hayo baada ya kushirikiana na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha baada ya kuonekana mapato
yaliyokusanywa awali kwa robo ratu za mwanzo kwa mwaka wa fedha kati ya 2023 na
2024 ni ndogo kulingana na vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya Halmashauri.
"Katika kipindi tajwa tumefanya uchambuzi wa mfumo mmoja katika eneo
la ukataji wa kodi ya zuio katika miradi ya maendeleo Halmashauri ya
Kibiti" amesema Kaimu Kamanda TAKUKURU Mkoa wa Pwani Sadiki.
Aidha kwa upande wa ufuatilia wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo tayari
wamefuatilia.kiradi kumi yenye thamani ya Bil.10,619,073,893.77 katika sekta za
Elimu, Maji,TANESCO, Afya,Ujenzi ,barabara na biashara kati ya miradi hiyo
hakukuwa na mradi ulioonekana kuwa na mapungufu.
Wakati huohuo TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeendelea na utekelezaji wa program
ya TAKUKURU Rafiki na kuzifikia kata sita huku kero zilizoibuliwa na kupatiwa
ufumbuzi zimetoka Idara ya Jeshi la Polisi, Utawala ,Afya , Elimu,Ardhi,TANESCO
na Barabara.
Kaimu Kamanda Sadiki amesema kuwa katika kipindi taja juu wamepokea
malalamiko 95 huku kati ya hayo malalamiko 55 yamehusu rushwa na taaifa hizo
zimeshughulikiwa kwa mujibh wa sheria kwa kuanzia uchunguzi ambao upo katika
hatua mbalimbali za uchunguzi.
"Taarifa 40 zilizobaki ambazo hazikuhusu rushwa zimeshughulikiwa kwa
njia ya uelimishaji,uzuiaji ushauri nankuhamishiwa idara nyingine, taarifa hizo
zimepokelewa kwa Mchanganuo ufuatao TAMISEMI 22,Mifugo/Uvuvi3,Elimu 4
,Polisi7,Ardhi12,Fedha3,Maji2,Mahakama 5,binafsi9, Ujenzi6,Afya7, Siasa
moja,Manunuzi moja,Maendeleo ya jamii moja,Kodi/ Mapato moja.
Katuka kipindi hiki TAKUKURU Mkoa wa Pwani imefungua jumla ya kesi mpya 11
Mahakamani huku kesi saba wametiwa hatiani.
Akizungumzia kuhusu namna walivyojipanga na vitendo vya rushwa katika
uchaguzi, "Mkoa wetu una ofisi tisa katika Wilaya zote kuna jumla ya Kata
133,Mitaa 490 na Vitongoji 2029, kwa kipindi hiki tumeshaanza kufanya
ufuatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika
baadaye mwaka huu".
Mwisho Kaimu Kamanda Sadiki ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani
kuendelea kuunga mkono jitihada za kufichua vitendo vya rushwa na wala rushwa
kwa kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kuwachukulia hatua wahusika hasa katika
kipindj hiki tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na
amewasisitizawananchi waonunua maeneo wahusishe serikali za mitaa na kufuata
sheria na kanuni na taratibu ili kuepusha migogo ya ardhi inayojitokeza mara
kwa mara na kwenda na kauli mbiu isemayo kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu
tutimize wajibu wetu.
0 Comments