Waombolezaji wakiwa mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Zainabu Mwangu (52) mkazi wa Misuna Manispaa ya Singida, anayedaiwa kufariki kutokana na kipigo cha mpenzi wake aliyekuwa akiishi naye.
......................
Na Dotto Mwaibale
MWANAMKE
Mmoja mkazi wa Misuna Manispaa ya Singida, Zainabu Mwangu (52) amefariki dunia
baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na mwanaume
aliyekuwa akiishi naye waliyemtaja kwa jina moja la Justine.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Misuna, Hamisi Lisu akizungumzia tukio hilo alisema
kwamba tukio hilo lilifanyika usiku wa kuamkia Agosti 6, 2024 ambapo jana
majira ya asubuhi alipigiwa simu na mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo
akimfahamisha kuwa katika mtaa wao kuna tukio na kabla ya kwenda eneo la tukio
alimpitia mkuu wa polisi wa kata hiyo na kwenda naye ,” alisema Lisu.
Alisema
baada ya kufika nyumbani kwa marehemu akiwa ameongoza na baadhi ya ndugu zake
marehemu akiwepo mama yake walimkuta Zainabu Mwangu ( Maarufu Mama Khadija) akiwa
amelala chini ya kitanda akiwa hana nguo na mwili wake ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali
na walipomuuliza kilichomsibu aliwajibu kwa shida kwa kutamka neno moja tu simu.
Alisema walimchukua
kwenda naye Hospitali ya Sokoine lakini alikuwa hajiwezi kutokana na kuwa na
maumivu makali na wakati akipatiwa matibabu alifariki.
Lisu alisema
asubuhi hiyo baadhi ya majirani kiwepo
baba ya marehemu walimuona mwanaume huyo aliyekuwa akiishi na marehemu akipiga
mswaki nje ya nyumba ya marehemu na walipomuuliza kuhusu hali ya mwenzake
aliwaambia kuwa hajambo.
Mjumbe wa
nyumba kumi wa eneo hilo shina namba 17, Rehema Athuman alisema kwamba
walipofika ndani walikuta fimbo ambayo ilikuwa imechanika chanika ikiwa na damu
na mwili wa marehemu ukiwa una majeraha ya kama mtu aliyekuwa amekatwa katwa na
kitu kama wembe hasa sehemu za tumboni, kifuani na maeneo mengine ya mgongoni.
Baadhi ya
wanawake wa mtaa huo wameonesha kusikitishwa mno na kitendo hilo kilichopoteza
uhai wa Zaituni ambaye wamesema alikuwa akifanya kazi nyumba ya kulala wageni
ya Buziluga iliyopo mjini Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polsi (SACP) Amoni Kakwale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa kamili ataitoa baadae.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii (SMAUJATA) Mkoa wa Singida, Ambwene Kajula alisema vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto havikubaliki hata kidogo na aatumia nafasi hiyo kulaani kitendo achofanyiwa Zainabu Mwangu.
0 Comments