Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Agosti 9, 2024 Makao Makuu ya NHC Upanga, Dar es Salaam.
.........................
Na John Bukuku
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi
amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) kwa kuanza utekelezaji wa mradi wa Samia Housung Scheme wenye lengo la
kujenga Nyumba 5,000, huku akisisitiza umuhimu wa kujenga nyumba hizo
katika maeneo ambayo bado hayafikiwa na mradi na yenye
uhitaji.
Akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Agosti
9, 2024 Makao Makuu ya NHC Upanga, Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, amesisitiza kutoacha malengo ya
kuanzishaji kwa Shirika la Nyumba la
Taifa lililoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere pamoja na
kujenga nyumba zenye viwango vya hali ya
juu ambazo zinaweza kununuliwa na wananchi wenye kipato cha chini.
Mhe. Ndejembi wakati umefika kwa NHC kuweka mipango ambayo itamsaidia mtu
mwenye kipato cha chini kumiliki nyumba za NHC kupitia utaratibu rafiki.
“Mnapaswa kuanzisha utaratibu wa kulipa kiasi fulani cha asilimia ya
gharama ya Nyumba na kuruhusu mteja huyo kuanza kuishi huku akiwa analipa kiasi
kidogo cha fedha kila mwezi mpaka atakapomaliza deni lake” amesema.
Mhe. Ndejembi ametoa wito kwa menejimenti ya NHC kuhakikisha hakuna wizi wa
vifaa vya ujenzi katika utekeleza miradi ya shirika la Nyumba jambo ambalo
litasaidia thamani ya Nyumba kuendana na gharama halisi.
0 Comments