Imeandaliwa na Dotto Mwaibale na Philemon Solomon
(0754-362990)
KATIKA hali
inayoonesha kuwiwa na maendeleo ya Singida, mkuu wa mkoa huo Halima Dendego
ameandaa mikakati kabambe ya kuukwamua ili kuufikisha kwenye nafasi ya juu kiuchumi.
Mikakati
hiyo ni pamoja na kuitisha kikao kazi kilichowahusisha viongozi wa mkoa, wilaya, Tarafa, pamoja na sekta
binafsi, chenye lengo la kuona viongozi
hao wanatoa michango yao mbalimbali itakayosababisha mabadiliko chanya katika
mkoa wa Singida.
Moja ya mkakati mwingine
aliousisitiza mkuu huyo wa Mkoa wa Singida ni viongozi kushikamana na kujituma
ili kuhakikisha Singida inafikia mafanikio yanayotarajiwa katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
“Kila mmoja wetu anatambua mwelekeo wa nchi, hususan dhamira ya dhati aliyo nayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania hivyo tunapaswa kuwa wamoja katika kuungajitihada hizo za Mhe. Rais kwa kufanya kazi kwa bidii,” alisema Dendego.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego katika kuonesha kuwa dhamira yake hiyo ni ya dhati ikiwa zimepita siku chache tangu alipoitisha kikao kazi hicho kilichofanyika Agosti 28, 2024 kuanzia leo Septemba 8, 2024 Mkoa wa Singida umekuwa Mwenyeji wa Maonesho ya saba (7) ya kitaifa ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Jitihada hizo za mkuu wa mkoa na dhamira yake hiyo
zinapaswa kuungwa mkono na wananchi wote wa Mkoa wa Singida ili kufikia nafasi
ya tatu kiuchumi nchini kwa kufanya kazi kwa bidii kuanzia maofisini, biashara, kilimo
cha vitunguu, alizeti, uwele, dengu,
viazi, mtama, mahindi na kwenye sekta ya
madini.
Kwa upande
wake Afisa Uhusiano wa Baraza la
Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC), Moses Kichogo alisema jumla ya taasisi 50
zitashiriki kwenye maonesho hayo na kuwa hakuna malipo yoyote isipokuwa kwa wale
tu watakao kuwa na meza za kuweka bidhaa zao.
Kichogo alitumia nafasi hiyo kuwaomba kuwakaribisha Wananchi wote wa Mkoa wa Singida kwenda kushiriki katika maonesho hayo ambayo ni muhimu sana yatakayofanyika Viwanja vya Bombadia Manispaa ya Singida na yatafunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) yatakayofanyika Septemba 10, 2024.
0 Comments