TUNAHITAJI SOBER HOUSE NCHI NZIMA

Subscribe Us

TUNAHITAJI SOBER HOUSE NCHI NZIMA

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati wa mkutano wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma 
 Septemba 11,2024.

Watanzania wamehimizwa kujitoa kuwekeza kwenye huduma za kuwasaidia waraibu wa Dawa za Kulevya kwa kuanzisha nyumba za upataji nafuu ili kuokoa nguvu kazi ya taifa iliyopotea kwenye dimbwi la matumizi ya Dawa haramu za Kulevya. 

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, wakati wa mkutano wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Sober houses) uliofanyika Dodoma leo Jumatano Septemba 11,2024.

Lyimo amesisitiza umuhimu wa kuongeza idadi ya vituo hivyo ili kukabiliana na tatizo la uraibu wa dawa za kulevya nchini. 

"Tunahitaji Sobar houses zaidi, hasa katika maeneo ambayo huduma hii haipatikani kwa urahisi. Idadi ya wateja wa dawa za kulevya nchini ni kubwa kuliko uwezo wa vituo vilivyopo sasa hivi", amesema

Kamishna Jenerali Lyimo amewataka wamiliki wa nyumba za upataji nafuu (Soberhouses) kuhamasisha wenzao kufungua vituo vipya, akibainisha kuwa kila mtanzania ana nafasi ya kuchangia katika juhudi za kupambana na uraibu wa dawa za kulevya 

"Kufungua Soberhouse sio lazima uwe umewahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya. Muhimu ni kufuata taratibu zilizowekwa na serikali", ameongeza. 

Kwa upande wao, wamiliki wa nyumba za upataji nafuu  wameeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo, ikiwemo ukosefu wa utambuzi na rasilimali za kutosha.

 Mwenyekiti wa mtandao wa wamiliki wa nyumba za upataji nafuu  Hamisi Shuwira, ameomba serikali kutoa vitambulisho vya utambuzi kwa wamiliki wa Sober houses ili kurahisisha kazi yao ya kuwasaidia wateja. 

Katibu wa mtandao huo, Saidi Bandawe, amesema ni muhimu kwa wamiliki wa Sober houses kufuata taratibu zilizowekwa na kutoa taarifa za mara kwa mara. 

Ameongeza kuwa kupambana na uraibu wa dawa za kulevya ni jukumu la kila Mtanzania, si serikali pekee.

Post a Comment

0 Comments