MIRADI YA MAZINGIRA KUMIMINIKA TANZANIA

Subscribe Us

MIRADI YA MAZINGIRA KUMIMINIKA TANZANIA

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika Mkutano wa Uwili na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF) wakati wa Mkutano 29 wa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaoendelea jijini Baku nchini Azerbaijan.

..........................................

Na Mwandishi Wetu

Tanzania inatarajia kunufaika na Dola za Marekani milioni 13 kwa ajili ya kuongeza wigo wa utekelezaji wa miradi ya kijamii kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Halmashauri 15 zaidi kupitia Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mitaji na Maendeleo (UNCDF). 

Hayo yamebainika wakati wa Mkutano Uwili baina ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na UNCDF uliofanyika wakati wa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaoendelea jijini Baku nchini Azerbaijan. 

Mkutano huo umelenga kujadiliana kuhusu maeneo ya ushirikiano zaidi katika miradi ya kijamii ya kuhimimi mabadiliko ya tabianchi ambapo kiasi hicho cha fedha kitatolewa kupitia utekelezaji wa Mpango wa Local Climate Adaptation Living Facility (LoCAL) na Kujenga uwezo wa Ufuatiliaji wa Fedha za Mabadiliko ya Tabianchi. 

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mhandisi Luhemeja amesema Tanzania itaendelea kunufaika na miradi hiyo katika sekta za maji, mifugo, uvuvi na miundombinu kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (NAP) na Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NDC). 

Wakati huo, Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) na NDC Partnership wamekubali kuongeza fedha zaidi za kuandaa na kutekeleza mchango wa taifa katika kupunguza gesijoto kqa kiasi cha zaidi ya Dola za Marekani bilioni 19.2 zinahitajika kuutekeleza. 

Itakumbukwa kuwa tayari Halmashauri tatu za Wilaya za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa zilizopo katika Mkoa wa Dodoma zilikwishanuifaka na mradi huo. 

Mkutano huo wa uwili uliwashirikisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Amina Khamis Shabaan, Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bi. Farhat Mbarouk, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Kanizio Manyika na wataalamu kutoka idara za kisekta na taasisi za Serikali.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika Mkutano wa Uwili na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) na NDC wakati wa Mkutano 29 wa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaoendelea jijini Baku nchini Azerbaijan.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) na NDC mara baada ya Mkutano wa Uwili wakati wa Mkutano 29 wa wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) unaoendelea jijini Baku nchini Azerbaijan. 

Picha ya pamoja
 

Post a Comment

0 Comments