Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Singida, Ustadh Omary Hamisi Mughenyi
..........................................
Na Mwandishi Wetu, Singida
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Ustadh Omary Hamisi Mughenyi, ameombwa
kuleta mageuzi makubwa na kuwaunganisha Waislamu ndani ya Mkoa wa Singida.
Hayo yamesemwa na Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro
wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha mwenyekiti huyo iliyofanyika Oktoba 15,
2025 mkoani hapa.
“Waislamu Singida tunahitaji ushirikiano wake, kuleta
mageuzi, kutuunganisha sanjari na kushirikiana na Serikali,” alisema
Alisema matamanio ya waislamu wa Mkoa wa Singida ni kuona
mabadiliko mapya ya mfumo kutoka kwenye Imani na kuelekea kwenye uchumi kwa
kuwahimiza watu kufanya kazi na kujitegemea.
Katika kikao hicho, ameahidi kufanya kazi kwa karibu na
viongozi wote wa mkoa na wilaya ili kuhakikisha taasisi ya BAKWATA inaendelea
kuwa chombo imara cha kusimamia amani, umoja, na maendeleo ya Waislamu mkoani
hapa.
Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali waandamizi wa Bakwata mkoani hapa walihudhuria wakiwepo Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Ustadh Omary Muna, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida, Mzee Chief Senge na Katibu wa Baraza la Wazee, ambapo kwa pamoja walijadiliana namna bora ya kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo.
Kikao cha ukaribisho kikifanyika
0 Comments