Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa,Rajabu Abdulrahman,akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman AAbudullah baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Tanga kwa ajili ya kilele cha madhimisho ya miaka 49 ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Februari 2, 1977 yataakaayo fanyika kesho Februari 5, 2026 wilani Muhuze mkoani humo.
...................
Na Dotto Mwaibale, Tanga
WANANCHI Mkoa wa Tanga wamejitokeza kwa wingi kumpokea Makamo wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman ambaye amewasili mkoani humo kwa ajili ya kilele cha madhimisho ya miaka 49 ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Februari 2, 1977 na kupokelewa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa, Rajabu Abdulrahman.
Mapokezi ya Makamo wa Pili wa Serikali ya Zanzibar ambaye pia na Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga ya lihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali huku akipokelewa Uwanja wa Ndege wa Tangu kwa burudani za ngoma za asili kutoka makabila ya mkoa huo.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Tanga Samweli Kiondo alisema leo usiku Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar atashiriki Maulid ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mohamad yatakayofanyika wilayani Pangani ambayo yameandaliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa, Rajabu Abdulrahman.
Kiondo alisema kesho Februari 5, 2026 Makamo huyo wa Pili wa Rais Zanzibar ambaaye atakuwa mgeni raasmi atahitimisha maadhimisho hayo Kimkoa wilayani Muheza kwa kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara.
Kiondo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho hayo ambayo yatafikia kilele chake kesho wilaayani Muheza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa, Rajabu Abdulrahman akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Dadi Kolimba.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa, Rajabu Abdulrahman akijadiliana jambo na Katibu wa Siasa Uenezi CCM Mkoa wa Tanga, Samwel Kiondo.







No comments:
Post a Comment