Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Danford Saimon akizungumza katika uzinduzi huo.
Diwani wa Kata ya Bassotu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Rose Kamili akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala akitoa taarifa ya mchakato mzima wa uundwaji wa jumuiya hizo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang, Paul Bura, akizungumza wakati wa uzinduzi wajumuiya hizo.
Wajumbe wa jumuiya hizo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Viongozi mbalimbali wakiwepo wa dini wakiwa kwenye hafla hiyo.
Muonekano wa keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya uzinduzi wa jumuiyahizo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilayaya Hanang, Janeth Mayanja akiwa katika picha ya pamoja na wakina mama pamoja na kikundi cha sanaa cha wanawake walioimba wimbo maalum wa uzinduzi wa vyanzo hivyo vipya vya maji.
WIZARA ya maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Kati imezindua
jumuiya mpya mbili za watumia maji zitakazokuwa na jukumu la kusimamia kisheria
na kutunza rasilimali za vyanzo vya maji vya Ziwa Bassotu na Bonde dogo la
Endagaw vilivyopo wilaya ya Hanang mkoani Manyara
Ongezeko la jumuiya hizo inafanya jumla ya jumuiya zote za
watumia maji zilizoundwa na bonde hilo kuzunguka Halmashauri zipatazo 40,
wilaya 32 ndani ya mikoa 8 nchini kufikia 9 mpaka sasa.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo hivi karibuni, Mkuu
wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayanja alipongeza hatua ya uanzishwaji wa jumuiya
hizo na kusisitiza pamoja na mambo mengine zitakuwa msaada mkubwa kwa usimamizi
wa uhifadhi endelevu wa vyanzo vya maji vilivyopo kwa manufaa ya wana-Hanang
Aidha, Mayanja alishauri wataalamu wa bonde la kati kufanya
tathmini ya kubaini vyanzo vingine vipya vya maji kuzunguka wilaya hiyo,
kikiwemo chanzo cha Endasaki na kuanza kuchukua hatua za mapema za uhifadhi
wake, ili kwa pamoja visaidie kutosheleza mahitaji ya maji ndani ya wilaya hiyo
kwa vizazi vya sasa na baadaye
Hata hivyo aliwasihi wanajumuiya wapya na viongozi waliochaguliwa
kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kushikamana,
ikizingatiwa kuanzia sasa kazi za usimamizi wa rasilimali za maji watakazozifanya
zipo kisheria.
“Fanyeni kazi zenu kwa kushikamana na pale mtakapokwamishwa
na yeyote msisite kuomba ushirikiano kutoka kwenye mamlaka nyingine zilizopo,
ikiwemo ofisi yangu na ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya ili kwa pamoja tuweze
kuvinusuru vyanzo vyetu vya maji
vilivyopo,” alisema Mayanja.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya bonde hilo,
Danford Samson alisema bonde la kati litaendelea kuanzisha zaidi jumuiya
nyingine kwa mujibu wa sheria lengo ni kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za maji
na utunzaji wa vyanzo vyote kuzunguka wilaya hiyo unakuwa endelevu.
“Ni jukumu letu sote kuvilinda, kuvitunza na kuvihifadhi
vyanzo vyetu vya maji vilivyopo ili viwe endelevu na vya kutosheleza kwa sisi
watumiaji wa leo na watakaozaliwa baadaye. Ikumbukwe binadamu tunaongezeka kila
siku lakini vyanzo ni vile vile haviongezeki, na vingine vimekauka kutokana na uvamizi
wa shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabianchi,” alisema mkurugenzi huyo
wa bonde la kati.
Awali, akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Hanang’ Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na Diwani wa Kata ya Bassotu Rose Kamili, alisema wananchi wa wilaya hiyo hususani wakazi waishio jirani na vyanzo hivyo, kwa moyo mkunjufu wameukubali mpango mzima wa usimamizi na uhifadhi wa kisheria wa vyanzo hivyo, chini ya jumuiya zilizoundwa na wako tayari kutoa ushirikiano wote kuhakikisha rasilimali za maji kwenye maeneo hayo zinalindwa na kuhifadhiwa.









No comments:
Post a Comment