MUME AMUUA MKE WAKE KWA KUMPIGA NA KITU KIZITO KICHWANI NA KISHA KUJINYONGA SINGIDA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, October 19, 2022

MUME AMUUA MKE WAKE KWA KUMPIGA NA KITU KIZITO KICHWANI NA KISHA KUJINYONGA SINGIDA



 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Lucas Mwakatundu, akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu tukio la mauaji yaliyofanywa  na Anthony Thomas Lugulu (41) mkazi wa Kijiji cha Ng'anguli Kata ya Maluga Wilaya ya Iramba mkoani Singida kwa kumuua mke wake Tatu Rashid (38) kwa kumpiga na kitu kizito  kichwani na kukipasua na kisha kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Lucas Mwakatundu, akiteta jambo na wasaidizi wake wakati akizungumzia tukiohilo la mauaji.

.....................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida.

 

ANTHONY  Thomas Lugulu (41) mkazi wa Kijiji cha Ng'anguli Kata ya Maluga Wilaya ya Iramba mkoani Singida amemuua mke wake kwa kumgiga na kitu kizito  kichwani na kukipasua na kisha kujiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Lucas Mwakatundu, akizungumza na waandishi wa habari jana alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 18, mwaka huu ambapo uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi kati ya wanandoa hao.

Mwakatundu akielezea tukio hilo alisema Oktoba 18, 2022 saa 2:30 usiku zilitokea taarifa za mauaji katika kituo kikuu cha polisi wilayani Singida kutoka kwa raia mwema katika mtaa wa Bima-Unyankindi kata ya Mitunduruni.

Alisema baada ya polisi kufika eneo la tukio alikutwa mwanamke aitwaye Tatu Rashid (38) akiwa amefariki ndani ya chumba chake huku mwili wake ukiwa na majeruhi yaliyotokana na kupigwa na kitu kizito kichwani.

"Timu ya wapelelezi kutoka Jeshi la Polisi ilipofika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa awali na kubaini kuwa mwili wa marehemu ulikuwa na jeraha kubwa kichwani lililotokana na kupigwa na kitu kizito huku mwili huo ukiwa umelala chali chini na kufunikwa kwa shuka na blanketi," alisema.

Alisema Oktoba 18, mwaka huu saa 12:56 asubuhi mume wa marehemu (Tatu), Antoni Thomas Lugulu naye alikutwa akiwa amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya uliofungwa kwenye mti nje ya nyumba yake.

Mwakatundu alisema katika eneo la tukio kulikutwa simu ya marehemu pamoja na ujumbe unaosema asibugudhiwe mtu yeyote kwa maamuzi aliyoyachukua.

"Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linatoa wito kwa wananchi kuachana na vitendo vya kikatili na kujichukulia sheria mkononi,wananchi wanatakiwa kuishirikisha jamii inayowazunguka,viongozi wa dini pamoja na wa serikali za mitaa kutatua migogoro yao ili itatuliwe kwa amani," alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad