Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti (katikati) akiwa mbele ya maaskofu wakati wa ibada ya kuwekwa Wakfu iliyofanyika Kanisa la Emmanuel Msalaba Mrefu Mjini Singida leo Oktoba 30,2022.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akivikwa pete ya kiaskofu katika ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akivikwa kofia ya kiaskofu katika ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akibarikiwa na maaskofu katika ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akikabidhiwa fimbo ya kiaskofu.
 |
| Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akimpongeza Msaidizi wake Mteule Mchungaji Dk. Zephania Nkesela wakati wa ibada hiyo, iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo nchini Dk.Fredrick Shoo.. |

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma hutuba kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Kwaya ya Matarumbeta kutoka Ujerumani ikitoa burudani.
Kwaya ikitoa burudani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba (wa tatu kutoka kulia) akiwa na viongozi mbalimbali katika ibada hiyo.
Kwaya ikitoa burudani.
Maaskofu wakiwa tayari kwa kumuweka Wakfu Askofu Mteule, Dk. Sprian Hilinti.
Wachungaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti akiwekwa Wakfu.
 |
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti (wa pili kulia)akipongezwa baada ya kusimikwa.
|
Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mhandisi Robert Kitundu akizungumza kwenye ibada hiyo.,
Waumini wa kanisa hilo wakimshukuru Mungu kwa tendo hilo.
Maaskofu wakitoa baraka kwa Askofu Mteule Dk.Sprian Hilinti.
Mke wa Askofu Mteule akimvika shada la maua mumu wake.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati Dk. Syprian Yohana Hilinti (katikati) akisaini hatiya utumishi.
Kwaya ikitoa burudani.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba (wa tatu kutoka kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) baada ya ibada hiyo.
Picha ya pamoja na wageni waalikwa kutoka Ujerumani.
Picha ya pamoja ya ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi hao wateule.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Picha ya pamoja na maaskofu.
Picha ya pamoja ndugu, jamaa na marafiki wa viongozi hao wateule.
Na
Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI
imesema itaendelea kushirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma
bora za maendeleo kwa wananchi hususani katika miradi ya elimu na afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameyasema hayo kwa niaba ya Rais Samia
Suluhu Hassan katika ibada ya kumweka Wakfu na kumsimika Askofu Mteule Dk.
Syprian Hilinti kuwa Askofu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kati
pamoja na kumwingiza kazini Msaidizi
wa Askofu Mteule Mchungaji Dk. Zephania Nkesela ibada iliyoongozwa na Askofu
Mkuu wa Kanisa hilo nchini Dk.Fredrick
Shoo.
“Serikali inatambua na kuthamini
mchango wa Kanisa la KKKT katika huduma za kiroho, kuhubiri injili
ya amani, umoja, haki na kweli” alisema Serukamba.
Alisema
kanisa hilo pamoja na kutoa huduma za kiroho linatoa pia huduma mbalimbali za
kijamii zikiwemo huduma za elimu na afya kwa kushirikiana na serikali akitolea
mfano huduma za Hospitali ya Ihambi iliyopo wilayani Mkalama ambapo Serikali
inawalipa mshahara watumisi 31 ili kuwezesha malengo ya kanisa kwa kutoa huduma
kwa wananchi bila ya kujali imani zao.
Akizungumza
baada ya kusimikwa rasmi kuwa Askofu, Dk.Sprian Hilinti aliipongeza Serikali
kwa kuendelea kuleta maendeleo kwa jamii
kama ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya VETA na kuwa jambo ilo linavumbua,
kulea na kutia moyo vipawa na kanisa litaendelea kuwatia moyo na kuwaambia watu
kuwa mambo yote yanawezekana.
Askofu Mkuu wa
Kanisa la KKKT, Dk. Fredrick Shoo akizungumza wakati wa ibada ya kuwasimika
viongozi hao wateule aliwataka
kuzingatia taratibu za kanisa katika uongozi wao na kujishusha wakati
wote badala ya kujikweza.
Aidha Askofu Shoo alitoa angalizo kwa
wanasiasa kuacha kujaribiwa kwa kuchukulia dini kama taasisi zisizo za
kiserikali kwa maana ya kuilinganisha dini na NGO’S.
“Nawaombeni msijaribiwe katika jambo hili iwe Kanisa au Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) msithubutu kuzifanya kama NGO’S” alisisitiza Dk.Shoo.
No comments:
Post a Comment