Na Mwandishi Wetu, Singida
SHIRIKA Lisilo la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) lenye
makao makuu yake mkoani Singida kupitia mradi wake wa Nilinde Project- lina
lenga Kupunguza matukio ya
ukatili wa kijinsia katika eneo la mradi ifikapo aprili 2024.
Maeneo hayo ya mradi ni Kata ya Irongelo
pamoja na kata ya Mrama katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi
huo wa Nilinde afisa mradi bw, Nice Daud aliseema mradi huo
utaangazia Ulinzi, Usalama na Upendo kwa wanawake na Watoto katika kata ya
Ilongero na Mrama.
Alisema
mradi huo ni moja ya mkakati wa uokoaji kwa wanawake na wasichana wanaoteseka
na kubaguliwa kutokana na kuathirika na ukatili wa kijinsia
Bw,Nice
alisema kuwa takwimu za ripoti ya benki
ya dunia juu ya tathmini ya ukatili wa kijinsia (March 2022) zinaeleza
Mkoa wa Singida ulishika namba 5 (31%). Wahanga wakubwa wa UWAKI ni wanawake
15-49
Kwa
mujibu ya taarifa ya ukatili wa kijinsia (Jan-December) 2021 kulikuwa na jumla
ya matukio 2,511 na vitendo viovu vilivyoripotiwa mkoani Singida.
Miongoni
mwa matukio hayo ni pamoja na Matukio 1,273 ya ukatili wa wanawake,Matukio 242
ya ukatili wa kihisia na,Matukio 996 ukatili wa kihisia.
Bw, Nice amesema kupitia shirika hilo la CIP mradi huo wa Nilinde Project-Lengo kuu ni kupunguza
matukio ya ukatili wa kijinsia katika eneo la mradi ifikapo aprili 2024 huku Malengo
mahsusi ni pamoja na kuimarisha uelewa wa jamii katika
kukabiliana na ukatili wa kijinsia,utekelezaji wa sharia na sera zinazowajibika
katika kulinda na kutekeleza haki za wanawake na Watoto.
Alisema
miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa usawa wa kijinsia mkoani
Singida ni pamoja kuwepo kwa mila potofu hasa, ukeketaji, utekelezaji mbovu wa
sheria na sera za ukatili wa kijinsia katika ngazi za chini,ukosefu wa uelewa kuhusu
usawa wa kijinsia miongoni mwa wana jamii jambo ambalo husababisha hatua duni
za usaidizi kwa wahasiriwa wa ukatili huo.
“mambo
mengine ni pamoja na kuhujumu mchakato wa kisheria na kutaka kumaliza mambo ya
ukatili kifamilia,ukosefu wa uelewa miongoni mwa wahanga au wahanga kuona aibu
kuripoti vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.”alisema Nice.
Bw,Nice
aliongeza kuwa katika mradi huo wa NILINDE miongoni mwa matokeo wanayotarajia
nipamoja na Kuimarisha miundombinu na
taasisi zilizopo zinazoshughurikia matukio ya ukatili wa kijinsia,kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaomiliki
rasilimali za mtaji na mali zisizohamishika katika jamii husika na Uboreshaji
wa maendeleo ya taasisi.
“Mikakati mingine tuliyonayo ni Kufanya utetezi na
uhamasishaji juu ya matukio ya ukatili wa kijinsia katika ngazi ya taasisi na
makundi maalum,Kuhamasisha na kuimarisha uwezo wa wanawake kuhusu haki zao za kumiliki
rasilimali na mali,Kushiriki katika mikutano na warsha za kujenga uwezo”
Kwaupande wake mkurugenzi wa Shirika hiko la CIP Bw,Afesso
Willson Ogenga amesema mbali na mradi huo wa nilinde shirika hilo limetekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo na ambayo imeleta matokeo tarajiwa kwa jamii na
shirika.
Bw, Ogenga alitaja baadhi ya miradi
ambayo shirika hilo linatarajia kutekeleza kwa mwaka 2022-2023 kuwa ni pamoja
na Kuboresha uwezo wa Watumishi wa Afya katika Utoaji Huduma,Fursa ya ufadhili
wa masomo ngazi ya Diploma kwa Wauguzi na Wakunga kutoka wilaya ya Singida kozi
ya mwaka 1,Mafunzo kuhusu afya ya mama na mtoto kwa wauguzi na wakunga kutoka
zahanati na vituo vya Afya.
Shirika la CIP kupitia mradi wa regional
cooperation kati ya mji wa Salzburg Austraria na Singida Manispaa tunaendelea
kutekeleza miradi ya elimu kwa Ujenzi wa vyumba vya madarasa mashuleni,Ugawaji
wa vifaa vya kujifunzia mashuleni.
Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi
huyo wa Nilinde mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida Bi,
Ester Chaula alisema mradi huo umekuja kwa muda muafaka kutokana na kukithiri
kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“nimradi ambao umekuja wakati sahii
kutokana na kuwepo kwa vitendo hivyo kwa kiasi kikubwa katika eneo letu hivyo
tukishirikiana kwa pamoja tutasaidia kuongeza mapambano”
“Sisi kama serikali tutatoa ushirikiano wa kutosha ilikufanikisha lengo la mradi huo ambapo kufanikiwa kwa shirika lenu ni sawa sawa na kufanikiwa kwa serikali”


%20Singida%20wakati%20wa%20zoezi%20la%20kutambulisha%20mradi..jpg)













No comments:
Post a Comment