WALENGWA 2517 WA TASAF CHALINZE WAKITHI VIGEZO VYA KUPATA RUZUKU YA UZALISHAJI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 3 November 2022

WALENGWA 2517 WA TASAF CHALINZE WAKITHI VIGEZO VYA KUPATA RUZUKU YA UZALISHAJI

Afisa Ufuatiliaji wa Miradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Janeth Mtelelah  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kuwatembelea na timu yake walengwa kadhaa wa TASAF na kukagua miradi yao mbalimbali ya ufugaji wa kuku, mbuzi na biashara ndogondogo katika ziara aliyoifanya leo Novemba, 3, 2022,  wilayani Chalinze.
Mratibu wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Michael Mwakanjuki akizungumza.
Mwezeshaji wa shughuli za TASAF katika halmashauri hiyo Flora Balakana akizungumza.
Mnufaika wa TASAF, Prisca Felix ambaye ni mfugaji wa kuku akuzungumzia mafanikio aliyopata baada ya kuwezeshwa na TASAF.
Mnufaika wa TASAF, Mwajuma Rashid ambaye ni mfugaji wa kuku na muuzaji wa mkaa akuzungumzia mafanikio aliyopata baada ya kuwezeshwa na TASAF.
Mnufaika wa TASAF, Prisca Felix ambaye ni mfugaji wa kuku akiwatoa nje kuku wake.
Mnufaika wa TASAF, Veronika Kumpite ambaye ni mfugaji wa mbuzi akiwa kwenye banda la mbuzi wake akifanya usafi.
Mnufaika wa TASAF, Veronika Kumpite akiwa amesimama na mjukuu wake mbele ya nyumba yake ya miti na udongo.
Mnufaika wa TASAF, Veronika Kumpite akiwa amesimama mbele ya nyumba yake mpya ya kisasa abayoanaijenga baada ya mafanikio kutokana na TASAF..
Mnufaika wa TASAF, Maria Msigala ambaye ni mfugaji wa mbuzi akiwa kwenye banda la mbuzi wake .
Mnufaika wa TASAF, Maria Msigala ambaye ni mfugaji wa mbuzi akiwa amesimama mbele ya banda la mbuzi wake
Wanufaika wa TASAF wa Kikundi cha Pain for Succes wakiwapa chakula bata wao wanaowafuga.
Wanufaika wa TASAF wa Kikundi cha Pain for Succes wakiwa katika picha ya pamoja kwenye shamba lao. Kushoto ni Mwezeshaji wao.
 Msanii Chozi Lukanga akigani shairi wakati wa ziaraya kutembelea kikundi hicho kilichopo Msata wilayani humo.
 

Wanufaika wa TASAF wa Kikundi cha Pain for Succes wakiwa katika picha ya pamoja  

Na Dotto Mwaibale, Chalinze, Pwani.

WALENGWA 2517 wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani wamekithi vigezo vya kupata ruzuku ya uzalishaji ambayo mpango wake mahususi ni kuwatoa  kwenye mpango wa TASAF ili waweze kujitegemea.

Hayo yabainishwa na Afisa Ufuatiliaji wa Miradi TASAF, Janeth Mtelelah wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwatembelea walengwa kadhaa wa TASAF na kukagua miradi yao mbalimbali ya ufugaji wa kuku, mbuzi na biashara ndogondogo.

Alisema walengwa hao 2517 ni kati ya walengwa 6,011 ambao walikithi vigezo vya kusoma na kupata shughuli za kufanya kama zilivyotajwa hapo juu kikiwemo kilimo ambapo waliomba fedha kuanzia Sh.100,000 hadi 500,000.

“Fedha hizi tunawapa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza tunawapa aslimia 50 kwa wafanyabiashara, asilimia 70 kwa wale wa mifugo na asilimia 60 kwa ajili ya wale wa kilimo na tumekuwa tukitoa kwa awamu ili kuweka uwajibikaji na kuweza kuwapima ambapo jambo la kushukuru kwa awamu ya kwanza walengwa 1960 miradi yao imefanya vizuri kutokana na timu yetu ya ufuatiliaji ambayo ilikuwa ikiwatembelea mara kwa mara” alisema Mtelelah.

 Alisema kuwa utaratibu uliotumika kutoa ruzuku hizo ni kwa kila mnufaika kuandika andiko lake la mradi na kisha kuomba fedha ambapo alipatiwa kulingana na vigezo vilivyobainishwa.

Mtelelah alisema hayo yote yanafanyika kwa uwezeshaji mkubwa anaoufanya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wa hali ya chini kwani kabla ya kuwawezesha walengwa hao baadhi yao walikuwa hawawezi kupata milo mitatu ambayo wanaipata hivi sasa ambapo pia wameweza  kuwapeleka watoto wao shuleni hakika ni kazi kubwa iliyofanywa na Mama Samia.

Alisema licha ya Rais kuelekeza fedha nyingi kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, ameona ni vema kutenga kiasi kikubwa cha fedha ikiwa ni pamoja na kutoa magari kwa TASAF nchi nzima  kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa kuzinusuru kaya za walengwa ambao kwa kiasi kikubwa unazisaidia kaya maskini kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

Mratibu wa TASAF katika halmashauri hiyo Michael Mwakanjuki alisema kazi kubwa ambayo wanaifanya ni kwa walengwa hao ambao wanapata fedha hizo kuhakikisha wanashirikiana na wataalamu ili miradi yao iende vizuri na kuinua uchumi wa kaya zao.

Alisema wataalam au wawezeshaji waliopewa mafunzo wamekuwa wakipita kwenye maeneo yao kutoa ushauri ili kukuza miradi yao.

Mwezeshaji wa shughuli za TASAF katika halmashauri hiyo Flora Balakana alisema katika shughuli za uzalishaji wamekuwa wakishirikiana na maafisa ugani katika vijiji 84 na kuhakikisha walengwa wao wote wanafikiwa na kupewa huduma stahiki ili waweze kutekeleza miradi yao.

Alisema mafanikio ya walengwa hao hayaji hivi hivi bali yanatokana na kazi kubwa wanayoifanya maafisa ugani kwa kushirikiana nao ambapo alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kwa kuwezesha kuwapeleka maafisa ugani kila kijiji ili kuwasaidia wananchi wakiwemo walengwa hao wa TASAF.

Baadhi ya walengwa waliotembelewa na miradi yao kukaguliwa ni Mwajuma Rajabu na Prisca Felix wakazi wa Msoga ambao wanafuga kuku, Veronica Kumpite (42) na Maria Msigala (60) ambao wanajishughulisha na ufugaji wa mbuzi katika Kijiji cha Mindutulieni.

Wanufaika wengine waliotembelewa ni Kikundi cha Wanawake cha Pain for Succes ambao wanaendesha miradi ya kilimo, ufugaji wa bata na sasa wanafyatua matofali kwa ajili ya kujenga banda la kuku ili waweze kuanzisha ufugaji wa kuku.

Wanakikundi hao ambao wanamoto wa maendeleo waliweza kutoa burudani ya nyimbo mbalimbali za kumshuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wanawake kupitia TASAF na shairi lililoimbwa kwa umahiri mkubwa na Msanii Chozi Lukanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad