CHONGOLO ATAKA WAZAZI KULINDA MAADILI YA WATOTO WAO

Subscribe Us

CHONGOLO ATAKA WAZAZI KULINDA MAADILI YA WATOTO WAO

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, akiwa amekalia kigoda wakati akihudhuria mkutano wa Shina namba 2 katika Kijiji cha Mtinko Wilaya ya Singida ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoaniSingida ya kuangalia uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo ziara alyoifanya Machi 3,2023. 

....................................................

Na Dotto Mwaibale, Singida 

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka Wazazi na Walezi nchini kusimamia na kuwaelekeza vijana wao kuzingatia suala la maadili hasa katika uvaaji wa mavazi yenye staha. 

Chongolo ameitoa kauli hiyo Wilaya ya Singida katika Kijiji cha Mtinko, baada ya Mzee  Emmanuel Mgoya kuelezea kukithiri kwa kumomonyoka kwa maadili kwa watoto wa kike na kiume katika  kikao cha Shina namba 2 ambacho alikihudhuria. 

"Katibu Mkuu wa CCM hivi sasa hali imekuwa mbaya Wanawake wanavaa  nguo zisizo na staha hali hii inanikera sana nakuomba ukamwambie Rais Samia Suluhu Hassan kuwa uku kwetu wanawake hawavai mavazi yenye staha" alisema Mngoya. 

 Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo akizungumza baada ya kuelezwa jambo hilo alisema waasisi wa taifa letu waliijenga nchi kwa misingi ya maadili, ambapo Wazazi na Walezi walitakiwa kuhakikisha  wanasimamia maadili ya watoto wao ili kuenenda vyema na utamaduni wa kitanzania. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba alisema tangu katibu mkuu huyo kuanza ziara mkoani hapa baadhi ya maagizo aliyotoa yameanza  kutekelezwa ndani ya siku nne tangu ayatoe ambapo alitaka yatekelezwe kabla hajamaliza ziara yake mkoani hapa.

Serukamba alitoa maelezo hayo katika mkutano wa Shina namba mbili uliofanyika Kata ya Mntinko wilaya ya Singida ambapo Chongolo alikuwa akisikiliza kero za wananchi.

Alisema Chongolo alitoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo ambapo akiwa wilayani Manyoni mmoja wa wananchi alielezea kero ya barabara mbili za mitaa wilayani humo kutotengenezwa kwa muda mrefu jambo lililokuwa likileta usumbusu kwa watumiaji..

"Katibu mkuu napenda kukueleza kwamba maagizo yako yote uliyotuelekeza tumekwisha yafanya zile barabara mbili za Manyoni tayari zimesembuliwa,saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi imekwisha nunuliwa na vituo vya kuchotea maji vikiwa vimefungwa na maji yameanza kutoka" alisema Serukamba.

Jambo jlingine alilolitolea maagizo ni ununuzi wa saruji kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa CCM wa wilaya hiyo ambapo alitoa fedha kwa ajili ya kununua saruji mifuko 200 huku Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota wakitoa ahadi ya kuchangia ujenzi huo mifuko 100.

 Changamoto nyingine iliyotolewa ni kukosekana kwa maji katika Kijiji cha Ulyampiti kilichopo Kata ya Unyahati wilayani Ikungi ambacho pamoja na maji kuchimbwa lakini yalishindwa kuwafikia wananchi kwa sababu ya kutofungwa vituo vya kuchotea majiambavyo gharama yake ilikuwa ni Sh.milioni 1.2 fedha ambazo zilipatikana kwa yeye kutoa Sh.Milioni 1 na mkuu wa mkoa kutoa Sh.200,000 ambapo aaliagiza kabla ya kumaliza ziara yake kazi hizo zimwe zimekamilika.

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhani Ighondo alitumia ziara hiyo kumuomba Chongolo asaidie ujenzi wa barabara ya lami ya kiwango cha lami ya kilometa 93 kutoka Singida mjini kupitia makao makuu ya wilaya hiyo Ilongero hadi Hydom mkoani Manyara.

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa Kijiji cha Ngimu, Kata ya Ngimu, Wilaya ya Singida ikiwa sehemu ya ziara ya kuimarisha chama pamoja na kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Vijana wa Itifaki wa CCM  Wilaya ya Singida wakimkabidhi ua Katibu wa CCM, Daniel Chongolo baada ya kuwasili Kijiji cha Mtinko kwenye ziara yake ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Ussi (Gavu) akihutubia wakazi wa Kijiji cha Mtinko wakati wa mkutano wa Shina namba 2 katikaziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ya kuimarisha Chama pamoja na kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida akiongoza kufanya itifaki katika mkutano wa Katibu Mkuu wa chama hicho Kijiji cha Ngimu.
Vijana wa Itifaki wa Wilaya ya Singida wakiwajibika wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Kijiji cha Mtinko.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida akiwasalimia wananchi kwakati wa mapokezi ya Chongolo katika kijiji hichocha Mtinko.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa Kata ya Ihanja Wilaya yaIkungi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji kupitia Jumuiya ya Wazazi na UVCCM, Ahmed Misanga (kulia) akiwa na kada mwenzie wa chama hicho wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Kijiji cha Mtinko.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Singida Ilongero ambayo katika Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo alipata fursa ya kuyakagua.
Wanawake wa Mntinko wakiwa wamejipanga foleni wakati wa kumpokea Katibu Mkuu Chongolo.
Wazee wa Mntinko wakiwa kwenye mkutano wa Shina namba 2 Mtinko.
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo (katikati) akikagua majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Singida Ilongero.akiwa ameongozana na viongozi wengine wa chama hicho. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlata.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo (wa pili kushoto) akiongoza hamasa wakati wa mkutano wa Katibu wa CCM, Daniel Chongolo uliofanyika Kijiji cha Ngimu


 

Post a Comment

0 Comments